Wednesday, September 26, 2012

WAANDISHI WA HABARI MBEYA WAPATA MAFUNZO YA ONLINE JOUNALISM

Mwenyekiti Mr Mjengwa ambaye ni mkufunzi wa mafunzo ya online Jounalism akiwa na Ally Kingo (kingotanzania.blogsport.com) pamoja na Joseph mwaisango (mbeyayetu)
Waandishi wa habari mkoani Mbeya wakiwa  katika picha ya pamoja


Nikiwa na wanahabari wa Mbeya wanaojifunza masuala ya Online Journalism niliwatangazia pia, kuwa Mjengwablog ambayo miongoni mwa wanahabari wale ni watembeleaji wake wakubwa inaadhimisha miaka sita ya kuzaliwa kwake. Siku ya kutimiza miaka sita ya Mjengwablog ilinikuta nikiwa vijijini kule Njombe na hakukuwa na uwezekano wa kutumia mtandao. Ni tarehe 19 Septemba.


 Naam, ilikuwa Jumanne, Septemba 19, 2006. Ni siku hiyo ndipo kwa mara ya kwanza niliingiza picha ya kwanza kwenye mjengwablog na kuashiria uzinduzi wa blogu. Ni picha hiyo inayoonekana. Niliipiga eneo la Kinondoni Shamba. Tangu siku ya kwanza, niliweka wazi kwenye fikra zangu, kuwa Mjengwablog iwe jukwaa litakalomtanguliza mtu wa kawaida. Iwe sauti ya ya wale ambao sauti zao hazisikiki. 


Ndio, nilidhamiria, na bado ni dhamira yangu, kuwa Mjengwablog iwe ni jukwaa la fikra huru. Kuwa iwe ni mahali kwa watu kutoa mawazo yao bila kukwazwa na mitazamo tofauti ya kiitikadi. Miaka sita imepita, nafurahia, kuwa bado naongozwa na dhamira hiyo. na http://www.mjengwablog.com/

Post a Comment