Wednesday, October 17, 2012

TANZANIA NA MALAWI KUNA AMANI JE MGOGORO WA MPAKA MCHAWI NI NANI?

WAKINA MAMA WA MALAWI WAKIELEKEA SOKONI ISONGOLE WILAYANI ILEJE KATIKA MKOA WA MBEYA- TANZANIA

WANANCHI WA MALAWI WAKIWA NA MAZAO YAO WAKIELEKEA SOKONI  ISONGOLE ILEJE

MAHINDI NDIO ZAO LA PEKEE KIPINDI HIKI NCHIN MALAWI (Hapo ni tahadhari ya kutoingia shambani lasivyo unalipishwa fain)

HAPA NIPO SOKONI NA WENYEJI WANGU WATU WA MALAWI NIKINUNUA MKATE KWA AJILI YA CHAKULA CHA MCHANA

SOKONI ISONGOLE ILEJE WANANCHI WA TANZANIA WANATEGEMEA MAHINDI YA MALAWI

SHEHENA YA MAHINDI YALIYONUNULIWA NA WATANZANIA KUTOKA KWA KWATU WA MALAWI

GHARA LA SERIKALI YA TANZANIA LILILOPO ISONGOLE ILEJE LIMEHIFADHI MAHINDI AMBAYO YAMENUNULIWA SOKONI HAPO KUTOKA KWA WATU WA MALAWI WANAOKUJA KUUZA

HAWA NI WATU WA MALAWI WAKIVUKA MPAKA ILI KUJA TANZANIA KUNUNUA NA KUUZA MAHITAJI YAO YA KILA SIKU.
UKIWA TANZANIA UNAPOSIKIA KUHUSU MGOGORO WA MPAKA WA MALAWI NA TANZANIA HUWA WATU WANAJIULIZA MASWALI MENGI SANA KUWA WATANZANIA WALIOPO MPAKANI NA WAMALAWI NI NANI JE NITOFAUTI NA WATU WALIOPO MIKOA YA KATIKATI YA NCHI ZAO?

NILIPO FANIKIWA KUFIKA KATIKA MJI WA ILEJE KATA YA ISONGOLE NILIKUTANA NA DARAJA MOJA KUBWA SANA LA CHUMA NA KUWAKUTA ASKALI WA USARAMA WAKILINDA NA KUWA HOJI KILA MTU ANAYEPITA HAPO NAMI NIKAUNGANA NA HUO MSURURU

KIUKWELI UKIVUKA DARAJA HILO UNAKUWA UPO NCHI JIRANI YA MALAWI TAYARI. LAKINI TOFAUTI SIKUIONA KUWA HAPO NA KABLA SIJAVUKA NA NILIPOJARIBU KUONGEA KISWAHILI WATU WA HAPO CHITIPA WALINISIKIA NA TULIELEWANA SANA NIKAWA MGENI WAO JAPO WATU WA HAPO CHITIPA WALIKUWA NA WASIWASI NA MIMI SANA KUWA NI MPELELEZI LAKINI NILIWAONDOA SHAKA

SHIDAYANGU ILIKUWA NI SWALI MOJA , JE MNAUJUA MGOGORO WA MPAKA ULIOPO KATI YA MALAWI NA TANZANIA?

JIBU LAO LILIKUWA NI MOJA KUWA HAWATAMBUI KITU WALA HAWAJUI ZAIDI YA KUSIKIA REDION. WANANCHI HAO WAKANIAMBIA KUWA KAMA HUO MGOGORO HUO UPO BASI NI WAVIONGOZI WAO HUKO JUU MAANA WAO KWA VYOVYOTE HAWATAHUSIKA NA HILO KWA KUWA WAO NI WATU WANAOTEGEMEANA NA WATANZANIA KWA KILA KITU

1. WANAMAHUSIANO YA KUOA NA KUOLEWA KWAHIYO WAO NI NDUGU WA DAMU
2. WANASHIRIKIANA KATIKA KILIMO NA BIASHARA
3. WANAONGEA RUGHA MOJA
4. WANATUMIA NETWORK MOJA YA MITANDAO

KWA UJUMLA KULIKUWA NA SABABU NYINGI SANA LAKINI MWISHO WAKASEMA WAO NI NDUGU NA HILO TATIZO NI LA WAO VIONGOZI NA MASLAHI YAO WANAYOYAJUA WAO,  SIO KWA WANANCHI WA CHINI MAANA MGOGORO HAUWAHUSU KABISA.

ZAIDI WAKAWAOMBA VIONGOZI WAO NA WATANZANIA WAKAE MEZANI WAJARIBU KUMALIZA TOFAUTI ZAO.

SAFARI YANGU SIKU HII ILIISHIA KWA KUKARIBISHA MAZIWA NA NYAMA YA MBUZI NIKAAMINI KUWA MALAWI NA TANZANIA WANA AMANI NA HUU MGOGORO NI WA VIONGOZI NA SIO WA WATU WA MAISHA YA KAWAIDA KAMA HAPA ISONGOLE ILEJE TANZANIA NA CHITIPA MALAWI.

KINGO
0752881456
Post a Comment