WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS PROFESA MARK MWANDOSYA AKIWA NA MKEWE LUCY MWANDOSYA WAKIJIANDAA KUMPOKEA RAISI KIKWETE. |
VIONGOZI MBALIMBALI WA MADHEHEBU YA DINI PIA HAWAKUWA MBALI KATIKA MAPOKEZI YA MHESHIMIWA RAISI KIKWETE. |
WANANCHI WAKIMSUBIRI MHESHIMIWA RAISI KIKWETE NJE YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SONGWE MKOANI MBEYA. |
VIJANA WA CHAMA CHA WAENDESHA BAJAJI JIJI LA MBEYA NAO HAWAKUWA MBALI KUMLAKI RAISI KIKWETE AMBAPO WALIKUWA NA MABANGO YA KUMSHUKURU NA KUMPONGEZA. |
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CRISPINI MEELA AKIMSIKILIZA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS PROFESA MACK MWANDOSYA. |
MKUU WA WILAYA YA ILEJE BI ROSEMARY SENYAMULE AKITETA JAMBO NA WADAU WA HABARI MKOANI MBEYA HUKU WAKIMSUBIRI MHESHIMIWA RAISI. |
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CRISPIN MEELA AKIBADILISHANA MAWAZO NA BAADHI YA WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA. |
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI AKISISITIZA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI WALIOJITOKEZA KUMLAKI MHESHIMIWA RAISI. |
MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI ( SUGU) CHADEMA NAYE HAKUWA MBALI KUMLAKI RAISI KIKWETE KATIKAT NI MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA |
MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBASI KANDORO AKITETA JAMBO NA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MBEYA ATANUS KAPUNGA. |
NDEGE ALIYOPANDA MHESHIMIWA RAISI IKIWASILI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SONGWE MKOANI MBEYA TAYARI KWA ZIARA YA SIKU MBILI. |
RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE AKITEREMKA KWENYE NDEGE BAADA YA KUWASILI KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA(SIA) |
AKISALIMIANA NA VIONGOZI MBALIMBALI |
BAADA YA KUVALISHWA SKAFU KUTOKA KWA VIJANA WA GREEN GUARD |
AKISALIMIANA NA WANANCHI |
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtoto mdogo muda mfupi baada
ya Kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe mjini Mbeya jana.(picha na
Freddy Maro)
Maelfu
ya Wakazi wa Mji wa Mbeya wakisalimiana kwa Shauku na Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa
Songwe mjini Mbeya tayari kuongoza sherehe za Mei mosi zinazofanyika
mkoani huko kesho(picha na Freddy Maro)
NGOMA ZA ASILI ZIKITOA BURUDANI |
AKIONDOKA KATIKA UWANJA WA NDEGE HUKU AKIWAPUNGIA WANANCHI MKONO. Picha na Jem .......................................................................................Bei ya mahindi Mbeya yaanza kuporomoka
Na Godfrey Kahango, Mwananchi
“Unajua mwandishi, wakulima wengi wameanza kuvuna
mazao yao kwa wingi hivyo hata sisi wafanyabiashara hatupati shida kubwa
sana kufuata mahindi hayo’’ alisema Israel ambaye anauza mahindi Soko
la Soweto.
Mbeya. Bei ya mazao mbalimbali jijini hapa imeanza kuporomoka. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa maeneo tofauti ulibaini kushuka kwa kasi bei za mahindi, ambapo debe moja sasa linauzwa kati ya Sh8,000 hadi Sh9,500, badala ya Sh14,000 hadi Sh15,000 za miezi iliyopita. Baadhi ya wafanyabiashara wa mahindi kwa nyakati tofauti walisema kuwa kushuka kwa bei ya zao hilo ni kawaida kutokana na msimu wa mavuno kuanza. Walisema licha ya kuwa wakulima wengi wameanza kuvuna mazao yao na kuwauzia wafanyabiashara, hata gharama za usafirishaji kutoka vijijini hadi masokoni nayo imepungua. “Unajua mwandishi, wakulima wengi wameanza kuvuna mazao yao kwa wingi hivyo hata sisi wafanyabiashara hatupati shida kubwa sana kufuata mahindi hayo’’ alisema Israel ambaye anauza mahindi Soko la Soweto. Lakini mfanyabiashara mwingine wa Kijiji cha Mahenje wilayani Mbozi, Rajabu Pwele, alisema kuwa kwa Wilaya ya Mbozi bei ya mahindi imeonekana kupanda. Alisema mwezi mmoja uliopita walikuwa wanauza debe moja Sh5,000 lakini hivi sasa wanauza debe moja Sh6,000 hadi Sh7,000. “Ni kweli huu ni msimu wa mavuno na wakulima wengi wameanza kuvuna mahindi yao, lakini huku kwetu bei inaonekana kupanda tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa Sh5,000 na sasa kutokana na wafanyabiashara wakubwa kuanza kuingia huku kwetu bei imepanda hadi kufikia kati ya Sh6,000 hadi Sh7,000,” alisema Pwela. Hata hivyo uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mbozi imewataka wakulima wilayani hapo kutobweteka na bei hiyo baada ya kuonekana kupanda na wakajiuzia ovyo ovyo na mwishoe wakajikuta wanakumbwa na balaa la njaa. ..................................................................................................... MOURINHO AFA KIUME SANTIAGO BERNABEU USIKU HUU, APIGA 2-0 LAKINI HAZITOSHI KUMSONGESHA FAINALI!!
Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Daah! Ali manusura vijana wa Mourinho waione Wembley mwaka huu baada ya kuwafunga nyuki wa kaskazini mashariki mwa Ujerumani, Borrusia Dortmund mabao 2-0 usiku huu katika dimba la Santiago Bernabeu
Matokeo
hayo yameitupa nje Real Madrid kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza
nchini ujerumani ambapo Mourinho alipiga kipigo cha mbwa mwizi cha mabao
4-1 na baada ya kushinda leo kwa mabo mawili Madrid wanatoka kwa
wastani wa mabao 4-3.
Mchezo
wa leo ulikuwa mgumu sana kwa Mourinho kwani walilazimika kumaliza
kipindi cha kwanza wakiwa 0-0 na kipindi cha pili kilipoanza bado mambo
yalikuwa magumu mpaka dakika ya 83 ambapo waliandika bao la kwanza
kupitia kwa Mfaransa Karim Benzema akipokea pasi nzuri kutoka kwa
Mjerumani Mesut Ozil.
Na
katika dakika ya 88 beki machachari Sergio Ramos alimalizia pasi
maridhawa ya Karim Benzema na kuzamisha gozi kambani, lakini matokeo
hayo hayajafua dafu kufuatia kipigo cha 4-1 ugenini.
Katika
kipindi cha kwanza cha mchezo huo Real Madrid walicheza vizuri zaidi ya
wapinzani wao lakini walishindwa kupangua ngome imara ya Kocha Flopp
aliyetamba toka awali kuwa hawataweza kuwafunga, lakini kipindi cha pili
waliachia na kufungwa, kama Madrid wangekuwa makini wangewatoa leo
baada ya kupoteza nafasi muhimu.
Ozil
hatasaulika kwa mashabiki wa soka wa Real Madrid baada ya kupoteza
nafasi muhimu za kufunga mabao ambayo yangewapeleka dimba la taifa la
Wembley nchini Uingereza kucheza mchezo wa fainali.
Waswahili
wana msemo wao usemao “Mwenzako akinyolewa zako tia maji”, Madrid
safari yao imekwisha leo usiku huku wakiathiriwa na matokeo ya mchezo wa
kwanza, watani zao wa jadi, FC Barcelona nao kesho wanapambana na
Wekundu wa kusini mwa Ujerumani FC Bayern Munich katika dimba la Camp
Nou huku Barca wakiwa na kumbukumbu ya kutandikwa mabao 4-0 Allianz
Arena.
Je
yatawafika ya Madrid leo ama watafunga mabao 5-0 ili wafuzu fainali na
hatimaye kukutana na Dortmund ambao wameshakata tiketi leo usiku.
Muuaji Robert Lewandowski akijaribu kupiga mpira kwa utalaamu mkubwa
Sergio Ramos akishangilia bao lake la pili lililowapa Madrid Matumaini makubwa
VIKOSI VYA TIMU ZOTE
Real Madrid: Diego Lopez, Essien, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Modric, Alonso, Di Maria, Ozil, Ronaldo, Higuain.
Subs: Casillas, Pepe, Khedira, Kaka, Benzema, Albiol, Morata.
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer, Gundogan, Bender, Blaszczykowski, Gotze, Reus, Lewandowski. Subs: Langerak, Kehl, Leitner, Sahin, Grosskreutz, Schieber, Felipe Santana. Mwamuzi: Howard Webb
Ramos akitandika mkwaju mkali kwa guu la dhahabu kwa wanasoka, guu la kushoto
: Benzema akiandika bao la kwanza
Wachezaji wa Real
Madrid wakimtaka kipa wa Dortmund Roman Weidenfeller asimame baada ya
kufunga bao la kwanza kwani alionekana kutka kupoteza wakati
Haikutosha: Cristiano Ronaldo hajaweza kuisadia Madrid kufika fainali ya UEFA mwaka huu
Robert Lewandowski akichungulia moja ya mashuti yake kama unaingia kimiani ama la
Hakuna Ujanja: Nyota wa Real Madrids Gonzalo Higuain akijaribu kumpokonya kipa Mats Hummels
Wakiruka juu zaidi: Lewandowski akipigania mpira na beki wa Madrid Raphael Varane
Ronaldo akionekana akilalamika baada ya kuungashwa
Hana jinsi: Mourinho akionekana amepaniki sana
Mwisho wa safari: Ronaldo akitembea uwanjani akionekana amechanganyikiwa na mwenye mawazo baada ya filimbi ya mwisho
|
No comments:
Post a Comment