Friday, September 6, 2013

HABARI NJEMA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA KUFANYIKA MBEYA


MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WENYE VIWANDA NA KILIMO TCCIA MKOANI MBEYA BWANA LWITIKO MWAKALUKWA AKIZUNGUMA NA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MBEYA 

AFISA MTENDAJI WA TCCIA MBEYA BI. ADELINA MUNAZI AMESEMA KUWA KUPITIA MAONESHO HAYO WANACHAMA WA TCCIA NA WANACHI WATAPATA FURSA YA KUTANDAA KIBIASHARA NA KUWATAKA WAYATUMIE VIZURI KWA MANUFAA YAO NA TAIFA KWA UJUMLA.


MOJA YA WAANDISHI WA HABARI CHARLES MWAKIPESILE AKIULIZA SWALI  KWA MWENYKITI WA CHAMA CHA WENYE VIWANDA





ZAIDI YA WAFANYABISHARA 400 KUTOKA NCHI SITA ZIKIWEMO ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA SADC WATASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA KIMAITAFA YA BIASHARA YATAKAYOFANYIKA NOVEMBA MWAKA HUU JIJINI MBEYA.
MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WENYE VIWANDA NA KILIMO TCCIA MKOANI MBEYA BWANA LWITIKO MWAKALUKWA AKIZUNGUMA NA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MBEYA AMESEMA LENGO MAONESHO HAYO NI KUWAPA FURSA WAFANYABISHARA WADOGO NA WAKATI KUKUZA BISHARA ZAO NA KUTANGAZA FURSA ZA UTALII ZILIZOPO UKANDA WA KUSINI MWA TANZANIA.
BWANA MWAKALUKWA AMESEMA KUWA MAONESHO HAYO AMBAYO YANADHAMINIWA NA TCCIA KWA KUSHIRIKINA NA WADAU WENGINE YATAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA JOHN MWAKANGALE JIJINI MBEYA AMBAPO WAJASIRIAMALI NA WANANCHI WA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI WATAJIFUNZA NAMNA YA KUFUNGASHA BIDHAA ZAO KUTOKA KWA WAFANYABIASHARA WENGINE WA WANACHI ZITAKAZO SHIRIKI AMBAZO NI TANZANIA, KENYA, ZIMBABWE,MALAWI, ZAMBIA NA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO (DRC).
NAYE AFISA MTENDAJI WA TCCIA MBEYA BI. ADELINA MUNAZI AMESEMA KUWA KUPITIA MAONESHO HAYO WANACHAMA WA TCCIA NA WANACHI WATAPATA FURSA YA KUTANDAA KIBIASHARA NA KUWATAKA WAYATUMIE VIZURI KWA MANUFAA YAO NA TAIFA KWA UJUMLA.

No comments: