ADHIBITIWA NA KITOTO KINACHODAI ALIKIBAKA, AKAKIAMBUKIZA VIRUSI
na Waandishi wetu
MBUNGE wa
Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), ameingia katika matata.
Katika kujaribu kudhibiti mtoto wa shule ambaye anadai alibakwa naye na
kuambukiwa virusi vya ukimwi, mbunge huyo ametoa vitisho vya kuua mtoto
huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili. SOMA ZAIDI ....
Siku moja
baada ya gazeti hili kuripoti habari za mbunge mmoja (bila kumtaja
jina), jana asubuhi Profesa Kapuya ameibuka na kumtisha mwanafunzi huyo
mwenye miaka 16 anayesoma Shule ya Sekondari Turiani iliyoko Magomeni
jijini Dar es Salaam.
Baada ya
kujua kuwa mtoto huyo ndiye alitoa habari za masahibu hayo, ambayo
mbunge hakutaka yajulikane, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma
meseji kadhaa za vitisho.
Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Profesa Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.
Alfajiri
saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993930, Profesa
Kapuya alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo: "chagueni kunisubiri tuje
tuongee au mnataka kufa?"
Baadaye
saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda
kwa mtoto huyo, ukisema: "Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama
za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi
ndo wenye nchi yetu.
"Mwambieni
Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si mmemuingizia hela
leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima
niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote.
"Jana si
wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa imeisha,
maana wameshatengeneza hela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu
wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani
anawakamata? Nani atapigana nasi?"
Hata
hivyo, baada ya kuhisi kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia hatua,
na wamewasiliana na taasisi mbalimbali za kiraia na serikali zenye uwezo
wa kumtia adabu, mbunge huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa kuonyesha
alikuwa anafikiria kunywa sumu..
Ujumbe
huo uliotumwa kwa mtoto huyo saa 11:2 3 ulisema: "nimwakosea sana, acha
nife mie nakunywa sumu nijiue, na nyie mje mnizike."
Hasira za
Profesa Kapuya dhidi ya mtoto hao zilitokana na hatua ya mtoto huyo na
dada yake kufichua unyama wanaodai kutendewa na mbunge huyo, ambaye
amewahi kushika nyadhifa kadhaa za uwaziri katika Serikali ya Awamu ya
Nne.
Tangu
alipogundua kuwa mtoto huyo alizungumza na gazeti hili juzi, saa 5:17
usiku wa kuamkia jana alituma ujumbe usemao: "Si mpo Bilz? Sasa tupo
pamoja na nyie mpaka usiku."
Baadaye saa 5:31 alituma ujumbe huu: "Hivi hamkubali kushindwa? Leo ulifuata nini ofisi ya CCM?"
Ujumbe
huo ulitokana na ukweli kwamba dada wa mtoto anayedaiwa kubakwa alifika
Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi asubuhi kuonana na Katibu
Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, ili kuomba chama kimsaidie
kumbana Profesa Kapuya, ambaye alikuwa ameanza kuwatisha yeye na mdogo
wake.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mtoto huyo, Kinana alisema suala hilo si la chama bali la Profesa Kapuya binafsi.
Mtoto
huyo alikataa ushauri wa kupeleka shauri hilo mbele ya vyombo vya
sheria, akidai kuwa jitihada zake zimekuwa zinazimwa na mbunge huyo
anayedai serikali haiwezi kumfanya lolote.
Alisisitiza
kuwa hana imani na serikali, lakini akasema yupo tayari kuchukua hatua
kali dhidi ya Profesa Kapuya iwapo atasimamiwa na watetezi wa haki za
binadamu.
Baadhi ya
mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki
za BInadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza
kumsaidia watoto hao, ambao ni yatima.
Mtoto
huyo na dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni,
walisema kwa sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania
kwa kuwa wamedhalilishwa, wametembezwa hadi Bungeni na wabunge bila
hatua kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika kituo cha polisi
Oysterbay tangu mwaka jana.
Hata
hivyo, kabla ya tukio la watoto hao kuripoti, ofisi za gazeti hili juzi
usiku kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku
wakiwatisha kwa simu na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia
tindikali.
Mmoja wa
watoto hao, alidai kuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wanawatisha juzi
walikuwa katika gari T170 BGY, Benz, Cream Metalic, ambayo inamilikiwa
na mbaya wao.
Jana
gazeti hili lilichapisha habari kuwa mwanafunzi huyo aliyesema kuwa
waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es
Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la
Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda
kuchua ada kwa mara ya pili.
Akizungumza kwa uchungu, alisema mbunge huyo alifanya kitendo hicho kwenye Hoteli ya Giraffe, Jijini Dar es Salaam mwaka 2011.
Alisema
kuwa yeye alikuwa na urafiki na mwanafunzi mwenzake Zuhura Mwaking'inda.
Mwaking'inda amewahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza Jimbo la Ubungo,
Jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa mwanafunzi huyo, rafiki yake (mtoto wa Mwaking'ida) alikuwa
amepooza hivyo alikuwa analazimika kumhudumia hali iliyowaunganisha hadi
huyo mtoto alipochukua jukumu la kumtambulisha kwa baba yake ambaye
naye alimtambulisha kwa Kapuya ili aweze kumsaidia fedha kwa jili ada.
Mwanafunzi
huyo alisema baada ya kutambulishwa aliitwa katika hoteli moja jijini
Dar ambapo baada ya kufika mapokezi wafanyakazi wa hoteli hiyo
walimkataza kuingia chumbani katika maana kwamba umri wake alikuwa mdogo
(mwaka 2011 alikuwa na miaka 14), lakini Kapuya aliamrisha aje chumbani
pamoja na dereva na kumwingiza kwa nguvu.
Akiwa
chumbani alimlazimisha kulala naye kisha kumpa sh laki saba, badala ya
sh elfu sitini na saba kiasi ambacho kilikuwa ndio mahitaji halisi ya
ada.
Mwanafunzi
huyo amesema baada ya muhula mmoja aliitwa tena na mbunge huyo katika
Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala tarehe 3 June 2012,
ambapo pia alimlazimisha kulala naye kwenye zulia la ofisi yake, kisha
kumpa sh 350,000/.
Alisimulia
kwamba wakati anatoka kwa huzuni ofisini kwa mbunge huyo, mmoja wa
wahudumu wa hapo alimuuliza kwanini anatoka kwa huzuni, alimweleza kisa
hicho, na huyo mama aliangua kilio kwa kumwambia "mwanangu umekufa pole
tu, huyu baba ni muathirika wa ukimwi".
Aliongeza
kuwa baada ya kuambiwa vile alilia na kufanya fujo hapo mapokezi hadi
alipokamatwa na walinzi wa kisha kupelekwa kituo cha polisi kufunguliwa
mashtaka, lakini akiwa polisi alipoeleza mkasa wote, Polisi walilazimika
kumwita Kapuya na wakawasuluhisha kwa makubaliano kwamba Kapuya atakuwa
anamlipia ada, na kumpa pesa za matumizi sh. laki tatu kila mwezi,
jambo ambalo amekuwa akilitekeleza kupitia simu yake ya mkononi
0755993930.
Kwa
mujibu wa mwanafunzi huyo, 24 Januari 2013, alifika mtu nyumbani kwao
mtu mmoja (jina tunalihifadhi) na kujitambulisha kuwa yeye ni jambazi na
kuwa alitumwa kwenda kuwaua kwa malipo ya sh. milioni 50, lakini
alipokuta ni watoto wadogo aliwasamehe, na kusema yeye ni jambazi sugu
hawezi kupoteza nguvu zake kuua vitoto.
Alienda
akiwa na bastola, maji kwenye chupa yanayodhaniwa kuwa ni tindikali na
bomba la sindano. Kwa mujibu wa mtoto huyo, jambazi huyo anasema kuwa
tayari alilipwa milioni 15 za awali.
Mtoto
huyo alisema jambazi huyo aliwambia kuwa yeye ni rafiki wa mtoto wa
Kapuya na wanamfahamu vizuri, lakini hataweza kuaua baada ya kubaini
kuwa wao ni yatima tu.
Hata
hivyo kufikia mwezi Februari mwaka huu, mtu asiyefahamika alienda
nyumbani na kutelekeza gari aina ya T.199 BGY Mercedes Benzi ya Blue
wakati wanafunzi hao wakiwa shuleni, kisha kuacha ufunguo kwa jirani yao
kwa maelekezo kuwa wakifika awapatie.
Na Kapuya
aliwapigia simu kuwaarifu kuwa amempa zawadi ya gari kwa ajili ya
matumizi ila yeye na dada yake wanaruhusiwa kuuza ili wapate pesa kwa
ajili ya mahitaji yake siku zilizosalia, kwani muda sio mrefu baada ya
uchguzi mkuu 2015, Kapuya atakuwa Waziri Mkuu, hivyo itakuwa ngumu yeye
kumtumia huyo binti pesa kama alivyoelekezwa na jeshi la polisi kituo
cha Oysterbay.
Baada ya
mwanafunzi huyo na dada yake ambaye ana umri wa miaka 20, kupewa gari
walishindwa kulitumia hivyo kutoa taarifa polisi kwani kwa kupokea gari
hilo ilikuwa ni kuwatelekeza kwani yeye hana hata hela ya kuweka mafuta
ya gari, hivyo walienda polisi ili kesi ipelekwe mahakamani kumshtaki
kapuya.
Polisi wa
Oysterbay walikubali kulipeleka tatizo hilo kwa Katibu wa Bunge, ambaye
alimwita mwanafunzi huyo na mdogo wake waende Dodoma kukutana na Kamati
ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ingawa walipofika Dodoma walikaa
na kamati ya hiyo kwa maelezo kuwa Kapuya hakuwepo hadi Bunge lilipoisha
walirejeshwa Dar es Salaam.
Mtoto
huyo na dada yake alitoka ofisi za CCM lakini akiwa anaelekea kituo cha
basi alithadharishwa na mwanafunzi mwingine kwa haraka kuwa akimbie kwa
kuwa atamwagiwa tindikali na watu waliokuwa wanamfuata nyuma,
alikimbilia katika mtaa wa Hoteli ya Star light kisha aliomba msaada
baada ya kupotea njia na hivyo alisaidiwa na mama mmoja kufikishwa
chumba cha habari cha Channel Ten.
Ni katika
chumba hicho ndio mwandishi wa habari hizi alienda na kuwakuta watu
wawili hao waliokuwa wanamhitaji binti huyo lakini walikatazwa
kumchukua.
- Imeandikwa Na Mjengwa Blog
.CHANZO TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment