MENEJA
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mbeya, Arnold Maimu amesema
wanaogomea kutumia mashine za Kielotronik(EFD) ni wafanyabiashara
wadogo ambao hata mashine hizo haziwahusu.
Aliyasema
hayo jana wakati akijibu swali kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi Dr.
Harrison Mwakyembe alipotembelea banda ya maonesho la Mamlaka hiyo
katika Maonesho ya Kimataifa ya kibiashara yanayofanyika katika viwanja
vya ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya.
Maimu alisema
wafanyabiashara wanaopaswa kutumia mashine hizo ni wake tu wenye uwezo
wa kuingiza Milion 14 pamoja na wafanyabiashara wote wenye viwanda,
biashara za jumla na rejareja, waliosajiliwa na ongezeko la thamani(VAT)
na wale wote ambao wataamuliwa na Kamishina wa TRA kutumia mashine
hizo.
Alisema
mara nyingi wanaoonekana barabarani na kupinga matumizi ya mashine hizo
ni wafanyabiashara ambao hawahusiki na wala hawajatajwa bali wanatumiwa
na wafanyabiashara wakubwa.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment