Tuesday, December 17, 2013

Andy Cole awapa nafasi U-17 wa Tanzania

.

colepix_282d6.jpg
Kulia Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Andy Cole amewaasa vijana walio chini ya miaka 17, kuongeza bidii ili kutimiza ndoto zao za kucheza kwenye timu kubwa duniani.

Cole ambayo yuko nchini, alisema: "Nimeona vipaji vingi Tanzania. Wachezaji wanaweza kabisa kuchezea klabu kubwa kama wataongeza bidii katika mazoezi yao.
Naomba nichukue nafasi kuwakumbusha wachezaji chini ya miaka 17 kuwa na nidhamu si ndani tu ya uwanja bali na nje ya uwanja kwani hiyo ndio nguzo ya mafanikio."

Katika hafla hiyo, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel iliipiga tafu timu ya taifa ya vijana ya U-17 kwa kuikabidhi mipira 100 ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuendeleza soka ya vijana nchi.


Mbali na hayo, Airtel iko katika mkakati mmoja na Serikali katika kuendeleza michezo nchini.
Akizungumza kabla ya kukabidhi mipira hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisema: Uwekezaji katika michezo ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inajipanga kushiriki katika mashindano ya kikanda na kimataifa."

Alisema kuwa kampuni yake inakabidhi mipira 100 kama sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kusaidia maendeleo ya michezo.

"Tutaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine na kuhakikisha tunapata mabalozi wazuri wa kutuwakilisha mashindano ya kimataifa."
Naye Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa amewashukuru Airtel kwa juhudi zake endelevu kusaidia michezo na kutoa wito kwa kampuni zingine kuiga mfano wa Airtel katika kusaidia michezo.

No comments: