Na Francis Godwi
MBUNGE
wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe amepongeza
jitihada kubwa zilizofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi (CCM)
chini ya Rais Dr Jakaya Kikwete katika kumaliza mgogoro wa mpaka
kati ya Tanzania na Malawi na kuwataka wananchi wanaoishi mwambao wa
ziwa Nyasa kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote.
Filikunjombe
alisema kuwa serikali ya Rais Kikwete ni serikali sikivu na ndio
sababu ya kulishughulikia suala hilo la mgogoro wa mpaka kwa wakati
zaidi bila kutokea machafuko ya aina yoyote .
Akizungumza
kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata ya Ilela na Manda wakati wa
ziara yake ya kusherekea pamoja na wapiga kura wake sikukuu ya
Krismas na Mwaka mpya juzi ,Filikunjombe alisema kuwa awali baada
ya kuwepo kwa taarifa ya Rais wa Malawi Joyce Banda kudai ziwa
Nyasa lote ni mali ya nchi yake ya Malawi wananchi wa Tanzania
wanaoishi jirani na ziwa hilo upande wa Tanzania walianza kuigiwa a
hofu kubwa .
Mbali
ya kuingiwa na hofu hiyo ya kiusalama ila bado walikuwa wakifanya
shughuli zao kwa hofu kubwa na baadhi yao kushindwa kuwajibika vema
katika shughuli za kimaendeleo kwa kuhofu vita kutokea .
Hata
hivyo alisema kutokana na serikali ya CCM kuwa sikivu zaidi
baada ya kubaini suala hilo mara moja jitihada za kulifanyia kazi
hilo bila kumwaga damu ilianza kufanyika na kuwa kwa sasa Rais
Kikwete amemaliza mgogoro huo na hakuna tatizo tena.
”
Ninawahakikishia wananchi wangu wa Manda na Ilela pamoja na kata
nyingine zote kama Makonde, Lifuma na zote ambazo zipo jirani na ziwa
Nyasa na wanategemea maisha yao kwa kuvua samaki na dagaa katika
ziwa hilo ….kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote” alisema
mbunge Filikunjombe huku akishangiliwa na wananchi hao
Alisema
kuwa Rais Kikwete amekuwa akijituma sana katika kuwatumikia
watanzania ila wapo baadhi ya watendaji wa serikali ambao ni
mzigo katika serikali yake na wamekuwa wakishindwa kuwatumikia
wananchi vema.
Filikunjombe
alisema yeye kama mbunge na mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Ludewa
kamwe hatakubali kuona wananchi wake wanakosa huduma za msingi
kama ilani ya CCM inavyosema kutokana na baadhi ya viongozi
kushindwa kutimiza majukumu yao vema.
Alisema
kuwa kwa kutumia fursa za ziwa Nyasa wananchi wa maeneo ya
mwambao mwa ziwa hilo wanaweza kujikwamua kiuchumi kwa kupatiwa
vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya uvuvi badala ya kuendelea
kuifanya kazi hiyo kwa kutumia vitendea kazi duni na kufanya uvuvi
wao kutokuwa na tija ya kimaendeleo.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi wenzake John Haule alisema kuwa awali
walikuwa na hofu kubwa ya kuendelea kufanya shughuli za maendeleo
kutokana na hofu ya kutokea vita ya mpaka kati ya Malawi na Tanzania na
kuwa hata wakati mwingine wakiona ndege zikipita angani
walikuwa wakiogopa kuwa yawezekana ni ndege za vita kutoka Malawi na
zinataka kuwaangamiza.
“Tunakupongeza
kwanza wewe mwenyewe mbunge wetu Deo Filikunjombe kwa kutuwakilisha
vema kwa Rais Kikwete na bungeni pia tunataka kuwaeleza viongozi wa
CCM sisi wana Ludewa tumechoka kuendelea kuwa na mbunge wa kipindi
kimoja kimoja sisi kwa sasa hatuhitaji mbunge mwingine zaidi yako
na kama watafanya wao watakavyo tupo tayari kuhama na wewe papote”
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha mbali ya
kuungana na mbunge Filikunjombe kuwahakikishia usalama wananchi hao
bado alisema kuwa ni vema wananchi hao kutumia mvua zilizopo kwa
kulima mazao yanayohimili ukame kama mihogo ambayo imekuwa ikistawi
zaidi katika maeneo hayo .
Kwani
alisema kuwa wataalam wa hari ya hewa wanadai kuwa hali ya mvua
kwa mwaka huu si nzuri sana pia upo uwezekano wa mwakani Taifa
kutokuwa na neema kutokana na wataalam hao katika uzoefu wao
kuonyesha miaka yote inayo malizika na namba 4 kuwa na tatizo la
neema.
|
No comments:
Post a Comment