KATIBU SIASA ITIKADI NA UENEZI MKOA WA MBEYA, BASHIRU MADODI,
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA
M,BEYA.
BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA MBEYA. |
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, anategemewa kuwa mgeni rasmi katika maazimisho ya miaka 37, ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) yanayotarajia kufanyika Jijini Mbeya.
Maazimisho hayo yanatarajia kufanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.
Katika maazimisho hayo, gwaride la heshima kutoka kwa vijana wa UVCCM, litapita mbele ya Rais Kikwete na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho na hatimaye kuchora michoro mbalimbali ya maumbo ya miaka 37 na mambo mengine kama ishara ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM
Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya, Katibu wa siasa itikadi na uenezi, Bashir Madodi, amewaambia kuwa sherehe hizo zinatarajia kufanyika Februari 2, mwaka huu badala ya Februari 5, kutokana na tarehe hiyo kuangukia siku ya kazi.
"Chama cha mapinduzi kitafanya sherehe za kutimiza miaka 37 kwa mwaka huu sherehe hizi zitafanyika tarehe 2/2/2014 kitaifa katika mkoa wetu na napenda kweka wazi ratiba kamili ya maamdalizi ya shughuri hiyo" alisema
Ratiba kamili ya sherehe hiyo tarehe 25-26/01/ 2014 maafisa wawili watawasili toka makao makuu na kuja mkoani Mbeya, tarehe 28/01/2014 Katibu NEC siasa na uenezi Nape Moses Nnauye atawasili katika mkoa wa mbeya.
Tarehe 30/01/2014 Makamu Mwenyekiti bara Philip Mangula Atawasili mkoani hapa na Tarehe 31/01/2014 atafanya ziara katika wilayaya Mbeya Mjini akiongozana na wajumbe wa sekretariet ya Taifa kuangalia uhai wa chama katika matawi yote na kuangalia utekelezaji wa iliani ya ccm pia atashiriki shughuri za ujenzi wa taifa.
Tarehe 01/02/2014 Kinana alakutana na wanachama wa ccm kutoka vyuo vikuu vilivyopo mkoani mbeya
Tarehe 31/01/ 2014 katibu mkuu wa CCM Abdala kinana atakutana na vijana wajasilia mali wa boda boda.
Tarehe 01/02/2014 Mwenyekiti wa ccm Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete atawasili katika mkoa wa Mbeya atapokelewa katika uwanja wa Ndege Songwe.
Tarehe 02/02/2014 Saa 12:00 mchana hadi 2:00 asubuhi yatafanyika matembezi ya mshikamano yatayo ongozwa na Mwenyekti wa ccm Taifa Ndugu Jakaya Mrisho kikwete yatakayo anzia soweto na kuishia ofisi za ccm mkoa wa mbeya
No comments:
Post a Comment