Wednesday, January 8, 2014

WANANCHI WA WILAYA YA RUNGWE NA MKOA WA MBEYA WAKIONGOZWA NA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE WAMZIKA KWA AMANI ASKALI S/STG BENADETHA OLOMI (TRAFIKI) ALIYEFARIKI AKIWA KAZINI KWA KUGONGWA NA GARI ENEO LA MCHANGANI TUKUYU WILAYANI RUNGWE

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKITOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA HASA WILAYA YA RUNGWE PIA KWA WANANCHI WOTE KWA KUSHITUSHWA NA KIFO CHA ALIYEKUWA ASKARI KATIKA KITENGO CHA USALAMA WA BARABARANI BENADETHA OLOMI (MAMA) BAADA YA MAUTI KUMKUTA AKIWA KAZINI MCHANGANI - ISONGOLE AMBAPO ALIGONGWA NA GARI ALIPOKUWA KASIMAMISHA GARI LINGINE LILILOKUWA LINATOKEA MBEYA KWENDA TUKUYU NA NDIPO GARI LILILO KUWA  LIKINDESHWA NA ERNEST NDOA KUTOKA WILAYA YA KYELA LIKAMGONGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. HIVYO CHRISPIN MEELA AMEWATAKA MADEREVA KUACHA KUENDESHA KWA KASI MAGARI SEHEMU ZA MAKAZI YA WATU NA SEHEMU ZA VITUO WANAPO SIMAMA ASKARI WA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZISIZO
ZA LAZIMA

1962 - 2014

MISA YA MAZIKO IMEFANYIKA KATIKA PAROKIA YA TUKUYU AMBAPO MAREHEMU ALIKUWA MWANA KWAYA KWAYA YA MTAKATIFU THERESIA. MISA IMEONGOZWA NA PAROKO MSAIDIZI PROJESTUS KAHITWA AMBAPO AMEWATAKA WATU KUJIANDAA KWA SAFARI YA MBINGUNI KWA KUTENDA MEMA HAPA DUNIANI, KWANI HAKUNA AJUAYE SAA WALA DAKIKA YA KUFA KWAKE HIVYO MUHIMU NI KUJIANDAA

BAADHI YA WATOTO WA MAREHEMU WAKIWA IBADANI KWA AJILI YA MISA YA KUMUOMBEA MAREHEMU MAMA YAO

KULIA PAROKO MSAIDIZI PROJESTUS KAHITWA AKIONGOZA MISA YA KUMUOMBEA MAREHEHEMU BENADETHA OLOMI

SAFARI YA KUELEKEA KAMBI YA POLISI TUKUYU MJINI KWA AJILI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU

MUME WA MAREHEMU MR EZEKEEL  TALABAN MWANDETELE

WATOTO WAMAREHEMU WAKITOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO KWA MAREHEMU MAMA YAO KIPENZI



ASKOFU WA DAYOSISI YA KONDE KKKT DR ESRAEL MWAKYOLILE AKITOA HESHIMA ZA MWISHO

AFISA USALAMA WA TAIFA WILAYA YA RUNGWE AKITOA HESHIMA ZA MWISHO

KUELEKEA NYUMBANI KWA MAREHEMU  MUMEWE KIJIJINI KWAO SYUKULA JUU KWA AJILI YA MAZIKO. NI KARIBU SANA NA KILELE CHA MLIMA RUNGWE

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED MSANGI AKIWEKA UDONGO KATIKA KABURI LA MAREHEMU BENADETHA OLOMI


HESHIMA ZA MWISHO ZA KIJESHI BAADA YA MAZIKO



HESHIMA ZA MWISHO ZA KIJESHI KWA MAREHEMU

KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED MSANGI AMEWATAKA NDUNGU NA JAMAA KUWA NA MOYO WA UVUMILIVU KWA KIPINDI HIKI KIGUMU, KWANI MUNGU ALIYETUPA BENADETHA NDIYE ALIYEMTWAA,  PIA AMESEMA KUWA HAKI ZOTE ZA MAREHEMU ZITAPATIKANA, WATOTO NA MUMEWE WA MAREHEMU WATAKABIDHIWAA

UFAFANUZI WA JINA LA MAMA AMBALO NI MAARUFU KWA MAREHEMU BENADETHA ULIANZIA KWA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA SYUKULA AMBAPO MZEE NASSORO HUMBO AMESEMA BENADETHA ALIKUWA MTU WA HURUMA NA MOYO WA KIPEKEE KWAKUWA KILA MTU WA KIJIJI HIKI AKIUMWA AU ANASHIDA YEYE AKIWA TUKUYU ATASAIDIA MATIBABU NA KUPATA POSHO . ZAIDI AMBALO HATASAULIKA KIJIJINI NI KUANZISHWA MRADI WA MAJI SAFI,  MRADI AMBAO UMEFANYA KIJIJI SASA KUWA NA MAJI AMBAYO  NI SAFI NA SALAMA,  HATA VIJIJI VYA JIRANI WANAPATA MAJI HAYO

NAYE MWAKIRISHI WA WASAFIRISHAJI BARABARA YA KYELA - TUKUYU - MBEYA MR FYANDOMO AMESEMA KUWA BENADETHA ALIKUWA NI KIONGOZI WA KIPEKEE SANA HADI AKAITWA MAMA,  KWA MAANA YA KUWA ALIKUWA AKIONA KOSA LAZIMA ATAKUITA  NA KUKUSHAURI PAMOJA NA KUKUPA ONYO,  TOFAUTI NA MAASKARI WALIOWENGI, KWANI WENGINGE HUTUMIA NAFASI ZAO KUWAKANDAMIZA MADEREVA NA WENYE MAGARI KWA KISA CHA KUWAKOMOA NA KUPENDA PESA ZA AIBU. HIVYO MAMA AMEFARIKI SASA TULIOBAKI TUIGE MFANO WAKE WA KUISHI NA WATU WA AINA ZOTE

JULIANA NANKOMA HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO TUKUYU AKITOA SALAM ZA RAMBIRAMBI

IBADA YA MAZIKO IKAFUNGWA KWA KUWASHA MISHUMAA KATIKA KABURI LA MAREHEMU BENADETHA OLOMI ALIYEZALIWA MWAKA 1962 NA ALIANZA KAZI KATIKA JESHI LA POLISI MWAKA 1982 NA AMEFARIKI AKIWA NA CHEO CHA S/SGT AKIWA ASKARI WA USALAMA BARABARANI. MAREHEMU AMEACHA MUME MMOJA NA WATOTO WATANO NA WAJUKUU WAWILI

MUONEKANO WA MIJI YA KKK NA SOGEA UKIWA KIJIJINI SYUKULA,  KIJIJI KILICHOPO MLIMANI RUNGWE.  PICHA HII IMEVUTWA SANA ILI KUONA KWA UKARIBU
KINGOTANZANIA
0752881456

No comments: