Februari 14 wapendanao duniani
huitumia siku hii kusherehekea na wapendwa wao wakijumuika kula na
kunywa. Mjengwa blog tunakuletea historia fupi ya siku hii ya wapendanao
aka Valentine's day
Asili
ya siku ya wapendanao "Valentine's Day" ni St Valentine, mhubiri wa
kikristo aliyekuwa akiishi karibu na mji wa Roma katika karne ya tatu
wakati wa utawala wa Claudis II.
Claudis alitaka awe na jeshi kubwa akategemea vijana wangejitolea na kujiunga na jeshi lake.
Lakini vijana wengi hawakupenda vita kwakuwa hawakutaka kuziacha familia zao na watoto wao.
Claudis akafikiria akaona hawa vijana
kuwakomesha waingie jeshini ni kupiga marufuku watu kuoana.Kuanzia hapo
akapiga marufuku watu kuoana akitegemea vijana hawatajali sasa kujiunga
na jeshi kwasababu ya familia zao.
Askofu Valentine naye kwa siri akawa anawafungisha ndoa vijana hao kwa siri.
Claudius aliposikia habari hizo aliamuru Valentine akamatwe na akahukumiwa adhabu ya kifo cha kunyongwa.
Wakati akiwa jela akisubiri siku yake
ya kunyongwa Valentine alikuwa akitembelewa na vijana waliokuwa
wakimpelekea maua kuonyesha wako pamoja nae.
Mmoja wa vijana waliokuwa wakienda
kumtembelea ni mtoto wa mkuu wa gereza ambaye aliruhusiwa kuingia mpaka
kwenye selo la Valentine "kupiga naye stori".
Inasemekana kwamba Valentine aliangukia katika mapenzi na binti huyo wa mkuu wa gereza wakati anasubiria kunyongwa.
Inasemekana kwamba muda mchache kabla
hajanyongwa Valentine aliomba kalamu na karatasi na kuandika meseji yake
ya kuaga akiweka sahihi "From Your Valentine" ( kutoka kwa Valentine
wako )
Valentine akanyongwa tarehe 14 februari mwaka 269 AD.
Baada ya kunyongwa kwa Valentine,
vijana wa Roma walianza kumuiga Valentine na kuwaandikia na kuwatumia
wanawake waliowapenda salamu za mapenzi.
Tangia siku hiyo tarehe hiyo ikaanza kuhusishwa urafiki, upendo na mahaba duniani huku ikihusishwa zaidi na mambo ya mapenzi.
Siku hiyo imezidi kuwa maarufu kila
miaka inavyoenda huku huku makampuni yakiigeuza siku hiyo kuwa ya
biashara zaidi kwa kufanya kila kitu maalumu kwa siku ya wapendanao
kionekane kuwa inabidi kiwe chekundu kuanzia kadi za salamu, maua, mpaka
nguo wavaazo wapendanao inabidi ziwe nyekundu.
Kuna watu wengi pia ambao
hawasherehekei siku hii kwa kuhoji umuhimu wa kuonyesha kumjali
umpendaye katika siku moja tu ya mwaka badala ya siku zote 365.
HAPPY VALENTINE'S
No comments:
Post a Comment