Thursday, February 13, 2014

MAZISHI YA YA AMBAKISYE RAMADHANI ALIYEFARIKI AKIWA KATIKA MAFUNZO YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA KIKOSI CHA RUVU YAMEFANYIKA NYUMBANI KWA BABU YAKE BARTON MWASAJONE UYOLE MBEYA ( 1993 - 2014)

MAZISHI YA YA AMBAKISYE ALIYEFARIKI AKIWA KATIKA MAFUNZO YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA KIKOSI CHA RUVU YAMEFANYIKA NYUMBANI KWA BABU YAKE BARTON MWASAJONE UYOLE MBEYA
 1993 - 2014
MAREHEMU AMBAKISYE RAMADHAN AMEFARIKI KATIKA HOSPTALI YA JESHI YA LUGALO DSM NA MWILI WAKE KUSAFIRISHWA MPAKA MBEYA UYOLE AMBAPO MAZISHI YAKE YAMEFANYIKA KWA BABU YAKE BARTON MWASAJONE MAENEO YA  UYOLE KATIKA MAKABURI YA NGOMBE

KIONGOZI WA MASAFARA WA KUTOKA KIKOSI CHA RUVU JKT AKISOMA WASIFU WA MAREHEMU AMESEMA KUWA AMBAKISYE ALIKUWA AKISUMBULIWA NA UGONJWA WA TUMBO AMBAPO MNAMO TAREHE KUMI ALIFANYIWA UPASUAJI NA KUKUTA UTUMBO UMEJISOKOTA UPASUAJI ULIOFANYIKA KWA MASAA NANE NA MAUTI YAKAMKUTA AKIWA ANAPEWA HUDUMA. FAMILIA YA MWASAJONE IMEACHWA NA MASWALI MENGI SANA JUU YA KIFO CHA AMBAKISYE BILA MAJIBU MAANA HAKUNA SIKU AMBAKISYE AMEWAHI KULALAMIKA KUUMWA UGONJWA WOWOTE HATA HILO TUMBO AMBALO LIMEPELEKEA KIFO CHAKE PIA KITU CHA AJABU NI USIRI WA TAARIFA ZA KUUMWA KWA MUDA MFUPI IKIWA AMBAKISYE TAREHE 9.02.2014 ALIONGEA NA SIMU NA MAMA YAKE MDOGO ANAYEISHI DSM AKIWA MZIMA LAKINI ASUBUHI YAKE ANAPEWA TAARIFA ZA KIFO CHA AMBAKISYE. LAKINI KWA IMANI YA FAMILIA IMEPOKEA TAARIFA HIYO KWA KUWA TAYARI AMBAKISYE AMEFARIKI TAYARI NA KUBAKI KUMRUDISHIA MUNGU SIFA NA UTUKUFU. AMEN

WANAFAMILIA YA MWASAJONE WAKIWA WANASIKILIZA KWA MAKINI TAARIFA YA KIFO CHA AMBAKISYE
BABU NA BIBI BARTON MWASAJONE WAKIWA KATIKA HALI YA HUZUNI KUONA MJUUKUU WAO AMEONDOKA KATIKA UMLI MDOGO SANA
MCHUNGAJI N.F R. MWALWEGA WAKIWA KATIKA HALI YA KUJIULIZA MASWALI YASIYO NA MAJIBU NA KUISHIA KUMSHUKURU MUNGU KWAKUWA MJUKUU WAO AMBAKISYE AMEFARIKI TAYARI
KULIA NI MWALIMU HANSI MWASAJONE AKITOA SHUKRANI KWA NIABA YA FAMILIA YA MWASAJONE KWA WALIOSAFIRISHA MAITI YA AMBAKIYE KUTOKA DSM  PIA WACHUNGAJI WANAOENDESHA IBADA YA MAZIKO , WATUWOTE WALIOHUDHULIA KATIKA MAZISHI PIA ALIWASHUKURU SANA VIJANA WALIOJITOLEA KUCHIMBA NYUMBA YA MILELE YA AMBAKISYE RAMADHANI
MJOMBA WA MAREHEMU ELIAS MWASAJONE AKITOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREMU AMBAKISYE
BIBI YAKE AMBAKISYE AMBAYE PIA NDIO MLEZI WA KE KWA MAJONZI AKITOA HESHIMA ZAKE ZA MWISHO KWA MAREHEMU MJUKUU WAKE
MSAFARA WA MAZIKO UKIONGOZWA KWA HESHIMA YA JESHI KUELEKEA KATIKA MAKABURI YA NGOMBE YALIYOPO UYOLE MBEYA AMBAPO AMBAKISYE ANAZIKWA


MWILI WA MAREHEMU UKISHUSHWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE
AMBAKISYE RAMADHANI ULIUMBWA KWA UDONGO, AMBAKISYE ULINARUDI KWA UDONGO MAVUMBI KWA MAVUMI, MWENYEZI MUNGU ATAKUFUFUA SIKU YA MWISHO. AMENI

MAZIKO YAKIENDELEA
BABA NA MAMA WA MAREHEMU AMBAKISYE RAMADHANI WAKIWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA MWANAO
BABU YAKE AMBAYE PIA NDIO MLEZI WA AMBAKIYE AKIWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA MJUKUU WAKE KIPENZI SANA
MAMA ZAKE WAKUBWA WAKIWA NA MAJONZI SANA WAKIELEKEA KUWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA MWANAO MPENDWA
WADOGO ZAKE NA KAKA ZAKE AMBAKISYE WAKIWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA NDUGU YAO MPENDWA
HESHIMA ZA MWISHO ZA KIJESHI KWA KWA MAREHEMU AMBAKISYE RAMADHANI
HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU
POKEENI BARAKA ZA BWANA KWA WALEWOTE MNAO MWAMINI NA KUMTEGEMEA MUNGU BWANA AWABARIKI NA KUWALINDA , BWANA AWAANGAZIE NURU ZA USO WAKE  NA KUWALINDA BWANA AWAINULIE USOWAKE NA KUWAPA AMANI KATIKA JINA LA YESU. AMEN
Post a Comment