MWENYEKITI
wa Kitongoji cha Lupembelwasenga, Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini,
kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Kibiki akikabishi kadi ya chama hicho kwa
Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini Delfina Mtavilalo, baada ya kutangaza
kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo
hilo, leo Machi 4, 2014 katika kijiji hicho.
Mngombea
ubunge wa jimbo la Kalenga Kupitia Chama cha Mapinduzi Bw. Godfrey
Mgimwa akizungumza na wananchi katika kijiji cha kikombwe katika kata ya
Lwamgungwe. Mngombea
ubunge wa jimbo la Kalenga Kupitia Chama cha Mapinduzi Bw. Godfrey
Mgimwa akipungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la
mkutano kijijini Kikombwe Mngombea
ubunge wa jimbo la Kalenga Kupitia Chama cha Mapinduzi Bw. Godfrey
Mgimwa akishiriki kucheza ngoma ya kihehe pamoja na msanii Dokii katika
mkutano huo.
Umati
wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wakisikiliza hotuba
mbalimbali za viongozi katika mkutano huo kijini Kikombwe.
*Asema kwa sababu ikiahidi inatenda
*Lakini Chadema porojo tu
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Lupembelwasenga, Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Kibiki, ameitabiria CCM kumiminiwa kura za kishindo na wananchi wa kitongoji hicho katika uchaguzi mdogo wa ubunge utakaofanyika jimboni humo Machi 16, mwaka huu.
Amesema, uhakika huo anao kutokana
na yeye na wananchi wengi wa kitongoji hicho kubaini kwamba CCM
ikiahidi jambo inatekeleza na ndiyo yenye ilani inayotekelezwa kwa sasa
tangu ilipopewa ridhaa na wananchi ya kuongoza nchi katika uchaguzi mkuu
uliopita, tofauti na Chadema ambao alidai ahadi zao ni za uongo na
hawana kazi ya kufanya katika shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti huyo wa kitongoji kwa
tiketi ya Chadema, alisema, hayo leo, Machi 4, 2014, kabla ya kutangaza
kuihama Chadema na kujiunga na CCM, katika mkutano wa hadhara wa kampeni
za CCM uliofanyika kwenye kitongoji hicho, kumnadi mgombea wa CCM,
Godfrey Mgimwa.
“Hivi sasa natangaza kuhama
Chadema, na nina kuhakikishieni kwamba wapo watu wengi nyuma yangu ambao
tumeachana na chama hicho na sote kwa jumla tumeahidi wananchi wa
kitongoji chetu kuifanya CCM iibuke na ushindi wa kishindo kwa kuimwagia
kura zetu nyingi katika uchaguzi huu, anayefikiri natania asubiri
ataona baada ya uchaguzi”, alisema Kibiki.
Kibiki alisema, yeye na wenzake
wameamua kuachana na Chadema baada ya kubaini kwamba, maneno ambayo
yamekuwa yakitolewa na viongozi wa chama hicho ni ulaghai mtupu ambao
ukifuatwa unawapotezea muda wananchi katika kujiletea maendeleo.
Alisema, baada ya kutafakari kila
mmoja kwa wakati wake, wamebaini kwamba, CCM ndicho chama chenye uhakika
wa kusimamia maendeleo yao, kwa sababu kiliwaahidi kujengwa barabara
nzuri na sasa ipo, mbali na mambo mengine ambayo yametekelezwa kupitia
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo la Kalenga na Waziri wa Fedha Dk. William
Mgimwa ambaye alifariki dunia Januari Mosi, mwaka huu.
Baada ya kutangaza kuachana na
Chadema na kujiunga na CCM, Kibiki alikabidhi kadi yake, kwa Mwenyekiti
wa CCM Iringa Vijijini Delfina Mtavilalo, hatua iliyofuatiwa na
wanachama wengine tisa wa Chadema kutoka kitongoji hicho nao kukabidhi
kadi zao kwa Mwenyekiti huyo.
Akizungumza na wananchi kwenye
mkutano huo, Mgombea wa CCM katika uchaguzi huo wa Kalenga, Godfrey
Mgimwa alisema, anatambua changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo
hilo, ndiyo sababu amejitolea kuipeperusha bendera ya CCM ili akipata
fursa ya kuchaguliwa asimamie kuzitatua.
Mgimwa alisema, miongoni mwa
changamoto ni uendelezaji wa ujenzi wa zahanati na shule katika
Kitongoji hicho, ambao ulikuwa umeanzishwa na Mbunge wa zamani Dk.
Mgimwa.
Alisema, ana uhakika kwa kupata
ushirikiano wa wananchi na mwongozo wa ilani ya CCM ya mwaka 2010, ana
uhakika changamoto hizo na nyingine zilizopo atapambana nazo hadi
kuhakikisha zinapungua au kwisha kabisa.
No comments:
Post a Comment