Friday, March 7, 2014

MWENYEKITI WA CHADEMA WANGAMA AJISALIMISHA CCM, ASEMA WENGI WAKO NYUMA YAKE

Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa Bw. Godfrey Mgimwa akishiriki kucheza ngoma pamoja na Mwenyekiti wa (CCM) mkoa wa Iringa Bi. Jesca Msambatavangu wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika kijiji cha Wangama kata ya Luhota mahali ambapo pi ndiyo alipozaliwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia (CHADEMA) Bi Grace Tendega, Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema katika kijiji hicho Bw.John Mgata amejisalimisha na kurejea CCM ambapo amesema wanachama wengine zaidi ya 50 wamekata shauri na wameamua kumfuata na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM). 2 
Msanii Dokii akitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ikuvilo kata ya Luhota. 5 
Viongozi mbalimbali na makada wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kijiji cha Wangama. 5A 
Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa Bw. Hassan Mtenga akimtangaza Mwenyekiti wa CHADEMA kijiji cha Wangama Bw. John Mgata mara baada ua kurejesha kadi na kujiunga na Chama cha Mapinduzi katika mkutano uliofanyika leo kijijini hapo 8 
Juliana Shonza kada wa CCM kutoka UVCCM Makao Makuu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Wangama kata ya Luhota mkoa. 9 
Wananchi wa kijiji cha Wangama wakipunga mikono yao juu wakati mgombea wa ubunge katika jimbo la Kalenga Bw. Godfrey Mgimwa hayupo pichanai  alipokuwa akiwahutubia
Post a Comment