Sehemu ya mlima unaolalamikiwa kumilikiwa na mwekezaji
Wananchi wa
kijiji cha Chalangwa Kata ya Chalangwa alfajiri majira ya saa kumi wamefunga
barabara ya Mbeya kwenda Chunya baada ya Jeshi la Polisi kumkamata Mohammed
Katembo kwa kosa la kutishia kuua.
Baada ya
kukamatwa Katembo nyumbani
kwake baada ya kufungwa pingu
akiwa chini ya ulinzi akidai sababu za kukamatwa kwake ilipigwa mbiu kijijini
hali iliyopelekea wananchi kujitokeza kwa wingi na kuamua kuifunga barabara
hiyo huku mtuhumiwa akitoroka akiwa na pingu mkononi.
Hali hiyo
ilisababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo wakiwemo abiria
waliokuwa wanakwenda na kutoka mikoa ya kaskazini,huku wananchi wakimtaka Mkuu
wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro aje kutatua mgogoro huo.
Mwenyekiti
wa kijiji Oscar Mwamwendesya amesema unatokana na mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la Joseph Mwazyele kupora eneo la mlima katika kijiji hicho bila taarifa
ya uongozi wa kijiji kupitia mkutano mkuu wa kijiji ambao ndio wenye dhamana ya
kutunza raslimali za kijiji.
Mkuu wa
wilaya ya Chunya Deotatus Kinawiro alilazimika kuingilia kati na kuifungua
barabara hiyo majira ya saa nne na nusu asubuhi kisha kukutana na wananchi wa
Chalangwa ambapo aliwataka kutoa kero zao ili kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.
Wananchi
walidai kuwa Mwazyele amekuwa akitumia Polisi kwa kuwakamata wananchi wanaohoji
juu ya umiliki wa machimbo katika mlima kijijini hapo hivyo wamekuwa wakiishi
kwa hofu lakini pia hawjui uhalali wa umiliki wake kwa kuwa kijiji hakina
nyaraka zozote.
Katika
mkutano huo Mkuu wa Wilaya alipiga marufuku tabia za kujichukulia sheria
mkononi ikiwa ni pamoja na kufunga barabara na mauaji yaliyokithiri kijijini
hapo na wilaya ya Chunya kwa ujumla na Jeshi la Polisi limekuwa likifanya kazi
kubwa kudhibiti hali hiyo.
Aidha
amepiga marufuku shughuli zote za machimbo kijijini hapo na Mohammed Katembo
ajisalimishe na pingu za Polisi lakini wananchi walikataa wakidai afunguliwe
papo hapo ambapo Mtuhumiwa alijitokeza na kufunguliwa pingu mbele ya Mkuu wa
wilaya.
Mkuu wa
wilaya alimaliza kwa kuwataka wananchi kuchangia shilingi elfu mbili kwa ajili
ya uwanja wa kisasa wa michezo hali ambayo wananchi waliafiki na kukubali
kuchangia.
Na Ezekiel Kamanga
|
No comments:
Post a Comment