Monday, April 7, 2014

UCHAGUZI JIMBO LA CHALINZE


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya mrisho Kikwete akisoma karatasi ya kupigia kura kabla ya kupia kura kumchagua Mbunge wa Jimbo la Chalinze kwenye kituo cha kupigia kura cha Zahanati Msoga.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kura yake ya kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze.

 Mama Salma Kikwete akiweka kura yake kwenye sanduku la kupigia kura kwenye kituo cha Zahanati Msoga.

 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha AFP Ndugu Ramadhani Mgaya akizungumza na waandishi wa habarai nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 1na kusema kuwa Chama chake kitakubali matokea yeyote na pia kama watashindwa watajipanga kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.

 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze Ndugu Mathayo Torongey akizungumza na baadhi ya mawakala alipotembelea kituo cha Ofisi Mtendaji Kata namba 1, Bwilingu.

 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete akihakiki taarifa zake kabla ya kupiga kura kwenye kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 3 Bwilingu, Chalinze.

Aziza mtoto wa mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akimsaidia Baba yake kuweka kura kwenye sanduku la kura ,Ridhiwani alipigia kura yake kwenye kata ya Bwilingu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Chalinze Ndugu Samuel Salianga akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata Bwilingu na kutoa tathmini ya jinsi zoezi linavyoendelea na kufafanua mambo mbali mbali yanayohusu uhalali wa wagombea kupiga kura popote ndani ya jimbo la uchaguzi.

wananchi  wa  jimbo la Chalinze   wamemaliza  kupiga  kura  hivi  punde  na  tayari  baadhi ya  vituo  matokeo  yameanza  kujulikana  huku  katika matokeo hayo ambayo  si rasmi mgombea  wa CCM Ridhiwani  Jakaya  Kikwete  anaendelea  kuongoza huku  vyama  vingine  vikimfuata kwa mbali  zaidi .

Hata  hivyo  zoezi   hilo  limefanyika katika  hali ya amani na utulivu na hadi  sasa  wananchi  wameendelea  kusubiri  matokeo  hayo kwa hamu  kubwa na baadhi ya  vituo  ambavyo  matokeo  yameanza  kujulikana  wafuasi wa CCM  wameanza  kushangilia .

Mbali ya  wafuasi wa CCM  kuonyesha  kuanza kushangilia  bado  wafuasi  wa  vyama  vikuu kama Chadema  na CUF  wameendelea  kujipa matumaini makubwa ya  kushida  katika  uchaguzi  huo na  kuwa  mwisho  wa zoezi la kuhesabu kura ndipo watakapo jua  mbichi na  mbivu  katika mchakato  huo 

 Tayari  Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha AFP Bw Ramadhani Mgaya ametangaza  msimamo  wa  chama  chake   baada ya matokeo hayo  kutangazwa kwa kudai kuwa atakuwa  tayari  kukubali matokeo hata kama atashindwa  katika  uchaguzi huo .

Mgaya  ambae amekuwa  mwanasiasa wa kwanza  wa  vyama  vya  upinzani  kuueleza umma kuwa  yupo  tayari  kwa  matokeo  hayo na  kutangaza  kujipanga kwa mwakani 2015  .
Wakati  mgombea  huyo wa AFP akieleza  hayo kwa upande wa  mgombea wa CCM 

Ridhiwan Kikwete  yeye  leo amefanya  kituko  cha karne  baada ya  kujipigia  kura  katika zoezi hilo na kisha  karatasi hiyo ya  kupigia  kura  kumpa mtoto  wake  mwenye  miaka  chini ya minne kuitumbukiza katika kisanduku  cha kuhifadhia kura 
uchaguzi  huo  unafanyika  kufuatia  kifo cha  aliyekuwa  mbunge wa jimbo  hilo kupitia  CCM Marehemu  Said Bwanamdogo aliyefariki  dunia mwanzoni mwa mwaka  huu .
Chanzo:Fransis G
Post a Comment