Licha ya
Serikali kupiga marufuku uuzwaji wa mazao ya wakulima bila kutumia vipimo
sahihi bado tatizo hilo limeendelea kuota mizizi katika maeneo mbalimbali
Mkoani Mbeya.
Baadhi ya
wakulima wanaoathiriwa na hali hiyo ni pamoja na wakulima wa
viazi,ndizi,mahindi,ufuta,mpunga,karanga,karoti na nyanya mazao ambayo hupimwa
kwa kutumia bakuli(ndonya) au debe na mara nyingine kujazwa katika
magunia(LUMBESA).
Hali imekuwa
na mbaya kwa wakulima hao kutokana na kutokuwa na Asasi ya kuwatetea na wafanya
biashara na wachuuzi kutumia fursa hiyo kuwafuata mashambani na kuwalipa ujira
mdogo na wengine kuwadhulumu wakidai watawalipa pindi mazao yatakapofika
Sokoni.
Baadhi ya
Wafanya biashara kutoka Mikoa mbalimbali wameanza kuingia Mkoani Mbeya na
kuwarubuni wakulima kwa kununua mazao yao mashambani mwao na wao kupata faida
mara tatu kwa kisingizio cha ukosefu wa usafiri.
Wakulima wa
viazi wa Kata ya Itewe ni miongoni mwa wakulima waliokumbwa na dhahama hii
ambapo kina mama ndiyo wamekuwa wahanga wakubwa kutokana na ukosefu wa pembejeo
wamejikuta wamegeuka watumwa kwa kulipwa shilingi elfu mbili tu kwa kuvuna
gunia moja la viazi.
Wameomba
Benki mbalimbali nchini kuwakopesha wanawake pembejeo za kilimo kwani wao ndio
wafanyaji kazi wakubwa shambani na wao ndiyo hutunza familia na wanao uwezo wa
kurudisha mikopo hiyo kwa wakati.
Ombi
limetolewa na wakulima hao ambao hawakupenda kutajwa majina yao kwa mamlaka za
vipimo waache kukaa ofisini bali waende mashambani ambako wakilima ndiko hupata
athari kubwa za kiuchumi.
Hivi
karibuni Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro alipiga marufuku vipimo vya
Debe na kuanza kutumia mizani hali iliyowafanya wakulima wa zao la ufuta
kunufaika zaidi licha ya kauli hizi kujirudia kila mala na kukosa usimamizi madhubuti ambapo mkulima hudhurumiwa mazao yake kwa vipimo vya kiunyonyaji .
Juhudi hizo
pia zimekuwa zikipiganiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe kwa zao la ndizi na
kahawa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Michael Kadege akipiga marufuku uuzwaji wa
kahawa mbichi.
|
No comments:
Post a Comment