Sunday, May 25, 2014

CCM YACHANA MBUGA MKOANI SINGIDA, YAELEZEA MIPANGO YAKE YA MAENDELEO KWA WANANCHI

19 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mjini Singida wakati alipowahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja vya Peoples mjini humo ambapo mawaziri mbalimbali wamehudhuria na kuwaelezea wananchi mpiango ya serikali katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 katika mipango ya maendeleo, Mkutano huu ulikuwa ni wa mwisho kabla ya kumalizia ziara yake katika mkoa  wa Singida hapo kesho kabla ya kuendelea na ziara hiyo katika mkoa wa Manyara keshokutwa , Ambapo katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye, Mawaziri waliohudhuria katika mkutano huo mkubwa ambao umerushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star Tv ni Dr. Charles Tizeba naibu waziri wa uchukuzi, Amos makala Naibu Waziri wa Maji, Mwigulu Nchemba naibu waziri wa Fedha na Uchumi na, Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Stephen Wasira Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) na Adam Malima Naibu waziri wa Fedha na Uchumi  na viongozi mbalimbali wa kitaifa na mkoa wa Singida.30 29 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Singida 27 
Aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Singida Mashariki Bw. Andrew Andalu akipongezwa na Mh. Stephen Wasira  mara baada ya  alipotangaza kukihama chama cha CHADEMA na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara mjini Singida, kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida mjini Khamis Nguli na Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu wa CCM.
26 
Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makala akiwahutubia wananchi wakati akiwaelezea kuhusu mipango ya serikali kuhusu maji katika mkutano wa hadhara mjini Singida. 24Naibu Waziri wa Uchukuizi Mh. Charles Tizeba akiwaelezea wananchi mipango ya serikali katika suala la ukarabati wa reli ya kati. 23 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa meza kuu na viongozi mbalimbali katika mkiutano huo. 22
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo. 21
Baadhi ya wanachama wa CCM kutoka Isuna. 20
Mkuu wa mkoa wa Singida Ndugu Parseko Kone akiwaelezea wananchi mafanikio yaliyopatikana katika mkoa huo chini ya ilani ya uchaguzi ya CCM.  17
Nyooomi33
Baadhi ya wananchi wakifuatilia matukio katika mkutano huo. 32 
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohamed Dewji akizungumza na wananchi wa jimbo lake f 15 
Msafara wa pikipiki ukielekea kwenye mkutano huo. 13
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulhman Kinana akishiriki kazi ya useremala wakati alipotembelea mradi wa kikundi cha vijana seremala kinachoitwa Aikande Workshop mjini Singida. 10 
Mitambo mipya ya maji katika mradi wa maji iliyofungwa katika kiiji cha Ng’aida manispaa ya Singida katika kupunguza tatizo la maji kwenye manispaa hiyo. 9 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulhman Kinana akimsikiliza mhandisi wa maji wa SUWASA Mhandisi Isaack Nyakonji wakati alipotembelea na kukagua mradi huo. 8
Mradi wenyewe12
Mh. Mohammed Dewaji akishiriki katika kupiga ripu kwenye shule ya sekondari ya Mughanga  mjini Singida 7 
Pendael Masai Afisa Muuguzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida  akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea hospitali hiyo kulia ni Mwigulu Nchemba Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi. 5 
Baadhi ya majengo ya hospitali hiyo.1a 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Dr. Doroth Gwajima mganga mkuu wa mkoa wakati alipowasili katika hospitali hiyo.

No comments: