Wednesday, August 20, 2014

IFAHAMU ASILI YA JINA TUKUYU.


Tukuyu Ni mji upatikanao kilomita 70 kutoka mbeya pia kilomita 61 kutoka kyela, Tukuyu ni Makao Makuu ya Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya. Ni moja ya maeneo yanayokaliwa na watu wa kabila la Wanyakyusa na ni Kabira ambalo linafahamika vyema kwa kilimo cha ndizi, maharage, mahindi, magimbi, viazi vitam na mvilingo na ufugaji wa mifugo mbalimbali na kadhalika kwani eneo hili hupokea mvua kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha masika na kwa sehemu kubwa zaidi ya mwaka.

Tukuyu ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani ikaitwa Neu Langenburg ("boma ndefu mpya") badala ya Langenburg ya awali iliyokaa mwambaoni wa Ziwa Nyasa ikazama chini wakati wa maji ya ziwa kupanda. Hadi leo jina la hoteli kuna hoteli iitwayo "Langiboss" inakumbuka jina la zamani. 

je asili ya mji huo kuitwa Tukuyu ni ipi?
 
Eneo ambalo leo uko mji wa Tukuyu lilikuwa na miti aina ya mikuyu.  Hivyo wenyeji wa sehemu hiyo ambao ni Wanyakyusa, wakawa wanapaita mahali hapo ‘patukuju’ yaani mahali penye miti ya mikuyu.  Kutokana na lafudhi ya Wanyakyusa, kwao ilikuwa rahisi kusema ‘tukuju’ badala ya ‘tukuyu’!”
 
Katika mwingiliano wa makabila mengi yaliyokuwa eneo hilo, wakiwemo wakoloni ambao walikuwa na majukumu ya kuweka kumbukumbu mbalimbali za maeneo nchini, neno ‘tukuju’ likabadilika na kuwa ‘tukuyu’ na hivyo kuwa jina la mji huo ulio kusini mwa Jiji la Mbeya katika barabara kuu iendayo mji wa Mbamba Bay ulio kando ya Ziwa Nyasa na nchi ya Malawi.

“Tukuyu ni jina zuri na halina matatizo ya kulitamka, japokuwa jina halisi lilikuwa ‘tukuju’ kama walivyokuwa wanalitamka watu wa asili katika eneo hilo,” anasema mwandishi huyo.


Karibu Tanzania, Karibu Rungwe mkoa wa Mbeya.

No comments: