Na Joseph Ishengoma
Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali
Hassan Mwinyi amesema serikali haijawahi kufuta Azimio la Arusha kama
inavyodaiwa na baadhi ya wananchi, bali ilizimua azimio hilo kuwapatia
viongozi wa kati uwezo wa kumudu makali ya maisha.
“Serikali haikufuta Azimio la
Arusha. Ililizimua azimio hilo kuwapatia viongozi wa kati kumudu makali
ya maisha, lakini baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia vibaya nafasi
hiyo kuvunja sheria ya maadili ya viongozi,” amesema.
Alhaji Mwinyi ameeleza hayo leo
jijini Dar es Salaam katika semina ya siku moja ya maandalizi ya sheria
ya kudhibiti mgongano wa maslai miongoni mwa viongozi na watumishi wa
umma iliyoandaliwa na Sekretarieti ya Maadili ya viongozi.
“Baadhi ya watu wamekuwa wakitumia
vibaya nafasi hiyo kuvunja maadili ya viongozi wa umma kwa kutumia
raslimali za umma kujinufaisha. Tabia hii imewafanya wananchi kutokuwa
na imani na viongozi wao,” amesema.
Kwa mujibu wa Alhaji Mwinyi,
mgongano wa maslai ini tatizo kubwa nchini linalotakiwa kuangaliwa kwa
umakini vinginevyo baadhi ya viongozi wataendelea kujinufaisha kwa
kutumia nafasi zao kazini.
Kwa upande wake Kamishna wa
Sekretarieti ya Maadili ya viongozi Jaji Salome Kaganda amesema lengo na
makusudi ya mapendekezo ya sheria hii ni kuleta amani na utulivu wan
chi.
Jaji Kaganda amesema, “mapendekezo
ya sheria hii hayalengi kuwafanya viongozi kuwa maskini, bali kasi yao
ya ukwasi iendane na halii halisi ya kipato chao.”
“Sheria hii itakapopitishwa na
ngazi husika, itapunguza ubinafsi wa viongozi walioko madarakani
kujipendelea wenyewe na maeneo wanayotoka,” amesema na kuongeza kuwa,
“Lazima kuwepo na hatua uya serikali kurejesha maadili ya maadili. Kama
itazingatiwa na kuheshuimiwa, taifa litafikia maendeleoo ya haraka
yaliyokusudiwa.”
No comments:
Post a Comment