MJUMBE
wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Prof. Mark Mwandosya ameeleza kuwa mpaka
ifikapo mwaka 2055 Tanzania itakuwa imeachana na umaskini katika nchi
ya uchumi wa kwanza endapo kutakuwa na dhamira ya dhati hususani kuwa
kuandika Katiba yenye kuleta nafuu kwa watanzania kwani kila kitu kwa
Waafrika kinawezekana pasipo kuwa na Wazungu.
Prof.
Mwandosya alisema hayo jana wakati akichangia mjadala wa katiba ndani
ya Bunge Maalum, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuwa na katiba
itakayozingatia vipaumbele ambavyo vinaweza kumkwamua mwananchi wa
kawaida kuondokana na umasikini na kuliinua Taifa kiuchumi.
Mhe.
Mwandosya amesema kuwa kuhusu changamoto na kero zinazohusu mambo ya
Muungano, katiba imejaribu kuzizingatia karibia zote, huku akieleza kuwa
hali ya Muungano ni imara na itaendelea kuwa imara.
Ili
kufanikisha nchi inapiga hatua baada ya kuwa na Katiba bora, Mhe.
Mwandosya amefafanua kuwa, watumishi wote wa Umma hawana budi kuliletea
tija Taifa hili kwa kuwa misingi imewekwa ndani ya rasimu ya katiba na
kusisitiza kuwa Mtumishi wa Umma sio mtawala na mambo yanayohusu miiko
na maadili ya mtumishi huyo yenye kumtumikia mwananchi serikali Katiba
imeweza kuyazungumzia.
“Tumezungumzia
kuhusu rushwa ambaye ni adui wa haki, kwamba hili tulitambue katika
Katiba ili katika Sheria likasimamiwe vilivyo na pia tumezungumzia pia
wale wanaouhujumu uchumi”, alisema Mhe. Mwandosya.
Kuhusu
haki za vijana, Mhe. Mwandosya ameeleza kuwa katika Rasimu ya Katiba
wamezungumzia juu ya haki za vijana, haki za walemavu, haki za wazee,
pamoja na haki za watoto, huku akiwashangaa baadhi ya wajumbe walioko
nje ya bunge hilo wanapotoa shutuma kuwa wanapoteza wakati kana kwamba
hawazungumzii mambo yanayowahusu wananchi.
“Nawaomba wananchi watusikilize na wayazingatie haya tunayoyasema”. Alisema Mhe. Mwandosya.
Akizungumzia
kuhusu Vyombo vya Usalama, amesema kuwa Katiba inawalinda na kuwatambua
viongozi wa usalama, ambapo sheria inawapa haki hata baada ya kustaafu
ili wakaweze kuishi maisha bora kwa kuchukua dhamana kubwa, hivyo kwa
dhamana hiyo viongozi hao wanapostaafu wanatakiwa kujiepusha na masuala
ya kisiasa kwasababu.
“Usalama
wa Taifa, Jeshi, Polisi, Magereza na Uhamiaji, hawa tunawatengezea
mambo mazuri sana wanapostaafu, kwahiyo tafadhari sana mkishatoka
tusaidieni, toeni ushauri lakini mkijiingiza katika siasa na mafaili
yetu huku mmeyashika hamtutendei haki”, alisema Mhe. Mwandosya.
Aidha,
ameomba kuwepo na Randama kwani hiyo inaandikwa katika lugha ambayo
mwananchi anaweza kuisoma tofauti na katiba kwani hiyo inaandikwa kwa
lugha ya kisheria, kwahiyo amependekezo kuwepo na randama kwa ajili ya
wananchi.
Mwandosya
ameongezea juu ya suala la amani kuwa ni jambo kubwa sana, amewananga
watu wenye tabia ya kutaka wananchi kuandamana wakapigwe risasi hao ni
watu wasioitakia mema nchi, hivyo amewaasa wananchi walipinge kwa nguvu
zao zote kuhusu suala hilo.
“Nina
ushauri kwa viongozi wenye kutaka wananchi wakapigwe risasi na Polisi,
naomba watangulie wao wajipige risasi, unapotaka kuwa Shujaa anzia
kwanza wewe mwenyewe, usiwapeleke vijana ambao ni matumaini ya nchi
yetu, ndugu zangu hili jambo siyo la busara hata kidogo na wananchi
mnapokwenda kuandamana, vijana mseme mnaandamana kwa nini? Kwasababu
gani? Na kwa misingi gani na kwasababu ya nani? Ukishajibu haya maswali
kwakweli mtaona nchi yetu kuwa ni nzuri sana, nchi ya amani”,
alisisitiza Mhe. Mwandosya.
No comments:
Post a Comment