Wednesday, October 8, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA JIMBO LA KILOLO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa Kilolo Mnadani waliojitokeza kumlaki katika ziara yake wilayani Kilolo Kinana yuko mkoani Iringa kwa ziara ya siku sita ya kikazi akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi, Ziara hiyo ina lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2014 na kuhimiza uhai wa Chama.

MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Profesa Peter Msolla akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya kikundi cha vijana cha Muungano ambacho kina jumla ya vijana arobaini waliopata mafunzo ya kufyatua matofali na ujenzi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Kilolo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Utengule kata ya Ihimbo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi Desemba CCM itashinda kwa kishindo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi  wa kijiji cha utengule kata ya Ihimbo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambapo aliwaambia viongozi wa Kata na Vijiji pamoja na ngazi ya wilaya wafanye mikutano na wananchi wao na waruhusu maswali ilikujua changamoto zinazowakabili wananchi .
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Utengule Ndugu Pancras Mkakatu ambaye ni mwanachama wa Chadema akiongea na wananchi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo  alimpongeza sana Katibu Mkuu wa CCm kwa kazi nzuri anayofanya na kueleza kuwa yeye ni CCM ila alitoka tu kwa sababu ya migongano na viongozi wengine wa CCM .
 Zahanati ya Kijiji cha Utengule ambayo imekamilika ilabado haijapata madaktari
 Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Uwindi Ndugu Charles Kigwile akiuliza swali linalohusu ujenzi wa madarasa ya shule hiyo ambao umesimama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhiwa mkuki kama ishallah ya kuwa Mtemi wa Wahehe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwashukuru wananchi wa kijiji cha Utengule kwa kumpa heshima ya kuwa Mtemi kwenye kijiji chao
 Katibu Mkuu wa CCM akiwa kwenye picha ya pamoja na Watemi wenzake wa kijiji cha Utengule.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaaga wananchi waliofurika kwa wingi kwenye mkutano wake.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mikono ya kwa heri na wananchi wa kijiji cha Utengule.
 Madarasa ya shule ya msingi Iwindi wilayani Kilolo mkoani Iringa
Mwalimu Josephine Konga wa Shule ya msingi akimuonyesha  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uchache wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo kiasi kupata shida sana katika kufundisha.

No comments: