Monday, October 27, 2014

PROFESA MWANDOSYA AJIPIGIA DEBE URAIS KWA NAMNA YAKE, ATAKA WANANCHI WAWAOGOPE WANAOTUMIA FEDHA.

Waziri wa Nchi Ofiri ya Rais, Profesa Mark Mwandosya, akiongea na baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya
BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu kuzungumzia mbio za urais katika uchaguzi wa Mwakani, Hatimaye Waziri wa Nchi Ofiri ya Rais, Profesa Mark Mwandosya, ameibuka na kutoa duku duku lake.
Profesa Mwandosya  amewataka Wananchi kuwakataa wanaotumia fedha nyingi kulazimisha kuchaguliwa kuwa viongozi wao na badala yake wao ndiyo wawapendekeze.
         
Alisema anashangazwa sana na baadhi ya Wanachama kutumia fedha nyingi kulazimisha kupendekezwa ili agombee uongozi ndani ya Chama na Taifa jambo ambalo alisema ni kinyume na utaratibu ambao waliuacha waasisi wa Taifa na Chama.
Alisema ndani ya Chama kuna vitu vingi vinavyoangaliwa ikiwa ni pamoja na kumteua mtu atakayegombea Urais lakini wakati huo huo atakuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa jambo ambalo wengi wao hawalitambui wanachojali ni kupata Urais pekee.
Alisema endapo wanachama wenzie watalitambua hilo litasaidia kuepusha mlolongo mkubwa ndani ya chama kwa kumteua mtu ambaye ataweza kudumisha fikra za Waasisi ikiwa ni pamoja na kuepuka migogoro isiyokuwa na faida yoyote kwa Wananchi.
Aliongeza kuwa Wananchi wanawajua watu wao ndani ya jamii  na kulinganisha na mfumo wa  ugomvi wa vijiji zamani ambapo Wananchi walikuwa wanamteua mtu ambaye ataweza kuongoza vita ya kukimboa kijiji kutokana na mapigano yanayokuwa yanaendelea.
Aliongeza kuwa mfumo wa sasa ni tofauti na mfumo iliokuwepo awali na mbao uliwekwa na waasisi pamoja na misingi ya vyama vya siasa ambapo hivi sasa kuna mtindo na imani kwamba fedha ndiyo msingi wa uteuzi na kuchaguliwa.
Alisema Watu wanatumia fedha vibaya kwa kuwanunua wajumbe, na kuwapa thamani wajumbe kwamba  mjumbe wa Mkutano mkuu thamani yake ni laki mbili, Mjumbe wa Nec Laki tano na Mjumbe wa Kamati Kuu thamani yake Milioni Moja.
Alisema hilo jambo Wananchi wanapaswa kulikataa kabisa na kama litaruhusiwa ikubalike kwamba maana ya siasa ni ya wenye fedha, sio ya wakulima na wafanya kazi, uongozi wa watu wenye fedha au mawakala waliowekwa na wenye fedha.
Aliongeza kuwa hiyo sio jadi iliyoachwa na Mwalimu Nyerere hivyo amewashauri wenye fedha nyingi kuzielekeza fedha hizo kwa wananchi kwa kuendeleza miundombinu ya afya, Elimu, maji na mahitaji ya jamii.
Aidha Profesa Mwandosya alijitolea mfano yeye mwenyewe kwamba hata ukijumlishwa mshahara wake tangu akiwa Waziri pamoja na safari za nje anazokwenda lakini bado hana uwezo wa kuhonga wajumbe wampitishe ili agombee urais.
Mwisho.

Na Mbeya yetu
Post a Comment