Monday, October 20, 2014

RATIBA YA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

tz}ccmv 
TAREHE SHUGHULI

19/10/2014 – 22/10/2014 Mikutano ya Wanachama wote wa CCM Matawini kwa ajili ya kuelimishwa na kuhamasishwa kuhusu Uchaguzi.
23/10/2014 – 25/10/2014 Kuchukua na kurejesha Fomu za kuomba kugombea Uenyekiti wa Mtaa, Kijiji, Kitongoji na Ujumbewa Serikali za Vijiji na Mitaa kwa Makatibu wa Matawi ya CCM.
26/10/2014 – 27/10/2014 Kampeni ya wagombea ndani ya Chama.
28/10/2014 – 29/10/2014 Wanachama wa CCM kupiga kura za Maoni za Wagombea Uenyekiti wa Kitongoji na Wajumbe wa Kamati ya Kitongoji kwenye Mashina yanayohusika.
30/10/2014 – 31/10/2014 Wanachama wa CCM kupiga kura za Maoni za Wagombea Uenyekiti wa Kijiji na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na vilevile kupiga kura za Maoni kwa Wagombea Uenyekiti wa Mitaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa kwa Mijini. Kura zitapigwa na wanachama wote wa CCM kwenye Matawi ya Kijiji au Mtaa husika.
01/11/2014 – 03/11/2014 Kamati za Siasa za Matawi kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Kata
04/11/2014 – 06/11/2014 Kamati za Siasa za Kata kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Kata na kwa Kamati za Siasa za Wilaya.
07/11/2014 – 09/11/2014 Halmashauri Kuu za Kata kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea Uenyekiti wa Vitongoji.
10/11/2014 – 11/11/2014 Kamati za Siasa za Wilaya kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Wilaya.
12/11/2014 – 14/11/2014 Halmashauri Kuu za Wilaya kufanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea Uenyekiti wa Mtaa, Uenyekiti wa Vijiji, Wajumbe wa Kamati za Mitaa na Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji.
15/11/2014 – 21/11/2014 Kuchukua Fomu na kurudisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
16/11/2014 – 21/11/2014 Mafunzo ya wajibu wa Wagombea na Mawakala.
24/11/2014 Siku ya uteuzi wa Wagombea kwa Msimamizi.

No comments: