Wednesday, November 12, 2014

AJALI MBAYA BASI LA WIBONELA LAPINDUKA NA KUUWA WILAYANI KAHAMA AKIWEMO DADA YANGU AMINA MWASEBA AKISAFIRI NA MUMEWE WAKIELEKEA DSM

TAREHE 24 07. 2014 IKIWA NI MIEZI MITATU TANGU AFUNGE NDOA NA MUMEWE LEO AKIWA NA MUMEWE WAKISAFIRI KUELEKEA DSM KWA HAFLA YA AMINA KUWA MFANYAKAZI BORA AMEPATWA NA AJALI NA KUFARIKI HAPOHAPO MUMEWE AKINUSURIKA KATIKA AJALI HIYO. DADA AMINA UMETUACHA KATIKA MAJONZI MAZITO WENZAKO KATIKA FAMILIA

NI NGUMU KUAMINI LEO LAKINI MUNGU NDIO KAAMUA HILI LITOKEE BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA NA LIHIMIDIWE

AMINA MWASEBA AKIWA NA MUMEWE SIKU YA SHEREHE YA KUMUAGA MJINI SUMBAWANGA KABLA YA NDOA YAO ILIYOFANYIKA 26.07.2014.
AMINA AKIWA NA MUMEWE KATIKA SAFARI YAO WAKIELEKEA DSM KWA HAFLA YA KUWAPONGEZA WAFANYAKAZI BORA WA FAIDIKA AKIWEMO NA AMINI MWASEBA  AKIWA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2014 NA MUMEWE AKIWA NI KIONGOZI WA FAIDIKA MKOA WA KIGOMA 

Huzuni na majonzi imetanda leo katika mji wa kahama baada ya bus la Wibonela Express linalofanya safari zake  Kahama -Dar kupinduka baada ya kutoka stand kuu ya kahama km chache toka stand katika eneo la Phantom  na kuua watu wanne.

Kwa taarifa za awali chanzo chz ajali hiyo ni mwendo kasi kufuatilia taarifa zetu. 
Wakazi wa Kahama wakiwa eneo la ajali leo asubuhi
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dkt Joseph Ngowi amesema watu waliopoteza maisha katika ajali ya basi leo asubuhi mjini Kahama ni wanne ambao ni Amina Emmanuel ambaye alikuwa mjamzito mkazi wa Kigoma, Salum (amefahamika kwa  jina moja) mtoto wa miezi mitatu Robin Jordan na mwanamme mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja huku majeruhi wakiwa 41.

Tukio hilo limetokea leo saa 12 asubuhi katika eneo la Phantom kilomita chache kutoka Stand ya Mabasi mjini Kahama baada ya  basi aina ya Scania lenye namba za usajili T 412 CGN mali ya Wibonela Ambalo lilikuwa likitokea mjini Kahama kwenda jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi kuendesha mwendokasi wakati akitoka katika kituo kikuu cha mabasi mjini Kahama na alipofika kwenye kona ya kutoka mjini Kahama kuelekea Isaka basi  lilimshinda huku yeye akiruka kutoka kwenye gari na kuangukia katika mtaro na basi  kupinduka.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dkt Joseph Ngowi  amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Maulid Shaban (44) mkazi wa Ushirombo, Athuman Issa (21) mkazi wa Kahama, Jordan Mbeya (28) mkazi wa Kasulu, Brandina Patrick (24) mkazi wa Kasulu, Oscar Lameck (19) Mkazi wa Kigoma, Stamili Shaban (38) mkazi wa Dodoma, Neema Dastan (18) Mkazi wa Kahama na Monica Gadson (35) mkazi wa Kahama.


Majeruhi wengine ni Nickson Andati ambaye ni Mchungaji mkazi wa nchi ya Rwanda (34) Lucas Mlezi (48), Joyce Fred (28) Asnati Remtula (27) , Eveline Hamis (6), Happy Hamis (30), Japhet Masha (29), Jackson Elisanto (26), Buligelila Ramadhani (40) na Rita Bryson (25) wote wakazi wa Kahama.
Pia kuna Irene Wilson (17) mkazi wa Kasulu, John Lembo(45) Mkazi wa Bariadi, Hamis Shaban (31) mkazi wa Kahama, Emmanuel Lambambo (32) mkazi wa Kigoma, Kashindye Masanja (28), Frenk Kishimba (21) Peter Bahati (22) wote wakazi wa Kahama, Iseme Ilila (36) mkazi wa Katoro Geita, Ebrania Saga (30) mkazi wa Kigoma, na Anika Amdani (35) Mkazi wa Kahama.
Wengine ni Shaban Omary (16) ambaye ni mkazi wa Dodoma,Grolia Moses (18) mkazi wa Kahama, Agnes Broto (35) Mkazi wa Ngara, Kulwa Said (40) mkazi wa Kahama, Peter David (42) mkazi wa Kahama,Tunga Lazaro (22) mkazi wa Mariadi, na Happy David (32) huku majeruhi wengine wakishindwakutambulika kutokana na kuwa mahututi.


Miili ya marehemu ipo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu

 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Post a Comment