HALMASHAULI YA RUNGWE YAOTESHA MICHE YA MITI MBALIMBALI NA KUIGAWA KWA WANANCHI NA TAASISI ZA SERIKALI NA BINAFSI.
AFISA MISITU WILAYA YA RUNGWE CSTOLY MAKEULA MWENYE DAFTALI AKIWA ANAGAWA MITI KWA WANANCHI MBALIMBALI WALIOJITOKZA KUPATA MITI BULE NA KUIPANDA KATIKA MANEO YAO |
WANAFUNZI MBALIMBALI WAKIONGOZWA NA SCAUT WAKIWA MAKINI KUPATA MICHE YA MITI KWENDA KUPANDA MASHULEN KWAO |
Tafiti
zinaonyesha kuwa takribani Hekta milioni 44 za misitu hupotea kila mwaka
nchini, ambayo ni hasara inayotokana na uharibifu wa ardhi, hasara hii
kubwa kwa Taifa hususan kwa mkulima aliyeko kijijini inahitaji matumizi
endelevu ya ardhi yatakayosaidia kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa
na ukame na kuongoa ardhi iliyoharibika.
WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA YAJIZATITI KULINDA MAZINGIRA KWA KUGAWA MITI
MBALIMBALI BILA MALIPO KWA WANANCHI WAKE
Wilaya ya Rungwe
kupitia ofisi ya mali asili imeotesha miche ya miti mbalimbali na kuigawa bila malipo yeyote
miche laki moja na thelathini kwa wakazi wa wiraya ya Rungwe kwa kujumuisha taasisi zote za kiserikali na taasisi binafsi pamoja na wananchi wa
kawaida ambao ni wakazi wa wiraya ya Rungwe.
Taasisi
zilizohusika ni pamoja na mahakama,shule za msingi na sekondari
vyuo,vivijiji, kata, makanisa, magereza na
takukuru. Na idadi ya wananchi walio husika katika kugawiwa miti ni
wananchi mia mbili kumi na nane. Na aina
ya miche iliyotolewa ni misindano ambayo ndio mingi zaidi, mipodo na miti ya matunda mbalimbali.
Idadi ya
miche iliyogawiwa mwaka huu imeongezeka ukilinganisha na mwaka jana
kwani miche ya mwaka jana 2014 ilikuwa miche laki moja na ishirini na mwaka huu
ni miche laki moja na therathini, hii inatokana na wananchi kutambua na kupata
uelewa wa kupanda miti.
Afisa misitu wilaya ya Rungwe Bwana Castory
Makeula amesema kwamba mwaka fedha wa 2014 na 2015
wameweza kufufua mashamba ya halmashauri yalioko simike yenye ukubwa wa hekta
kumi kutokana na bajeti waliyokuwa wamepewa na kupanda miche elfu nane ya miti.
Bwana Castory ameomba Serikali kupitia Halmashauri
ya wilaya Rungwe kuongeza bajeti katika mwaka wa
fedha wa 2015 na 2016 ili kuweza kufufua mashamba mengine ya Halmashauri ili waweze
kupanda miti mingi zaidi kwani mahitaji ya wananchi kupanda kiti wilayani Rungwe ni makubwa ukilinganisha na miche ya miti mbalimbali inayozaliswa kwa sasa.
TUMAIN OBEL
KINGOTANZANIA
No comments:
Post a Comment