Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Simba kabla ya mpambano wa Fainali
ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya Mtibwa Sugar katika kusherehekea miaka
51 ya Mapinduzi ya Zanzibar mchezo uliofanyika jana Uwanja wa Amaan
Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Kikosi
kamili cha Timu ya Simba kikiwa katika picha ya pamoja Uwanja wa Amaan
Studium jana wakati wa Mpambano wa mchezo wa fainali ya kombe la
Mapinduzi Cup na Timu ya Mtibwa Sugar mchezo huo ikiwa ni kusherehekea
miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
[Picha na Ikulu.]
Wananchi na Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia kwa makini mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi Cup kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliochezwa jana katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambapo simba iliweza kutokakifua mbele kwa kuwafunga Mtibwa matuta 4-3, [Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Simba Hassan Izhaka baada ya
kuifunga Mtibwa kwa matuta 4-3 mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi
uliofanyika jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya
Zanzibar katika uwanja wa Amaan Studium,[Picha na Ikulu.]
Wachezaji
wa Timu ya Simba wakisherehekea ushindi wao baada ya kuwafunga kwa
matuta timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa fainali ya
kombe la Mapinduzi 4-3 katika uwanja wa Amaan studium Mjini Unguja jana
katika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na
Ikulu.]
Mashabiki
wa Timu ya Simba Wengundu wa Msimbazi walipokuwa katika jukwa la Saa
katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja wakishangilia timu yao
ilipocheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika fainali ya kombe la
Mapinduzi,Timu hiyo ya Simba ilishinda kwa matuta 4-3ikiwa ni
kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na
Ikulu.]
Bendera
ya Shirikisho la mchezo wa Mpira wa Miguu FIFA iliyobebwa na Vijana
wakiwepo na waamuzi wa Mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya
Timu ya Mtibwa Sugar na Simba katika Uwanja wa Amaan Studium katika
kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika mchezo
huo Simba iliibuka kwa ushindi wa matuta 4-3 dhidi ya Mtibwa, [Picha na
Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk (kushoto) wakiangalia mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi Cup kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliochezwa jana katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambapo simba iliweza kutokakifua mbele kwa kuwafunga Mtibwa matuta 4-3 , [Picha na Ikulu.]
No comments:
Post a Comment