Saturday, January 17, 2015

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (KAZI MAALUM), MHESHIMIWA PROF. MARK MWANDOSYA ATEMBELEA BWAWA LA KUZALISHA UMEME LA MEROWE DAM ELETRICITY COMPANY SUDAN

Merowe Dam wakati wa ujenzi Sudan
Mhe. Prof. Mwandosya akipata maelezo kutoka kwa Wataalamu wa Merowe Dam Electricity Company
Mhe. Prof. Mwandosya alipata nafasi ya kuongea na waandishi wa Habari wa Sudan walioongozana na ujumbe wake
Mhe. Prof. Mwandosya alipata nafasi ya kuongea na waandishi wa Habari wa Sudan walioongozana na ujumbe wake
Picha ya pamoja kati ya Ujumbe wa Mhe. Prof. Mwandosya na Uongozi wa Merowe Dam Electricity Company

Prof. Mwandosya akipata maelezo ya mitambo ya kufuatilia uzalishaji umeme inavyofanya kazi


Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini Sudan jana tarehe 15 Januari, alitembelea moja ya miradi mikubwa ya kuzalisha umeme kwa kutumia mabwawa ambao unaendeshwa na Kampuni ya Merowe Dam Electricity Company.
Mradi huu ambao uko Kaskazini mwa Nchi ya Sudan umejengwa  kwa gharama ya USD 2.0 millioni ambapo Serikali ya Sudan imechangia 30% na zilizobaki ilikuwa misaada na mikopo kutoka kwa wafadhili wanje.
 Mradi umejengwa kando kando ya Mto Nile na una uwezo wa kuzalisha 1,250 megawati ambayo ni inachangia 60% hadi 70% ya mahitaji ya nishati ya umeme nchini Sudan.
Mhe. Prof. Mwandosya alipata nafasi ya kutembelea mradi ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Merowe Dam Electricity Company, Bw. Mahgoub Eisa Khalil alimtembeza sehemu mbalimbali za mradi kama inavyoonekana katika picha zifuatazo.

No comments: