Thursday, January 15, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA TABORA

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora kuhakikisha umefanya mkutano na wananchi ili kufanya makubaliano jinsi ya kusimamia mradi wa umeme wa kontena ili wananchi waanze kunufaika mara moja.
unnamed1 
Mtendaji wa kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora Gundi Igonzo (kulia aliyevaa koti la kijani) akitoa maelezo juu ya mradi wa umeme wa kontena kijijini hapo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati)
unnamed2 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kampuni ya kusambaza umeme katika wilaya ya Uyui na Mirambo ya Chico – CCC ya China mara baada ya kutembelea eneo palipohifadhiwa vifaa kwa ajili ujenzi wa miundombinu ya umeme katika wilaya za Uyui na Mirambo.
unnamed3 
Mtaalamu kutoka Kampuni ya Chico – CCC, Luo Xiaoyong (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) juu ya hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika wilaya za Uyui na Urambo mara Waziri alipotembelea eneo palipohifadhiwa vifaa kwa ajili ya kazi hiyo.
unnamed4 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisalimiana na wakazi wa Inala mkoani Tabora kabla ya kufanya mkutano nao ili kusikiliza kero zao.

No comments: