AKITOA TAARIFA YA SERIKALI KWENYE BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA RUNGWE MKUU WA WILAYA YA RUNGWE AMESEMA KUWA WILAYA YA RUNGWE IMEFIKIA ASILIMIA 95% YA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MAABARA |
MOJA YA MAABARA ZILIZOJENGWA KATIKA SHULE YA SEKONDARI TUKUYU |
PAMOJA NA UJENZI ULIPOFIKIA KWA 95% NI ASILIMIA TANO TU ZIMEBAKI KUKAMIRISHA UTENGENEZAJI WA SAMANI NA KUPATIKANA KWA VIFAA VYA MAABARA |
KIWANGO CHA UFAURU KWA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA RUNGWE IMEFIKIA 73% KITAIFA |
Agizo la
Mheshimiwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr Jakaya Mrisho
Kikwete la kujenga maabara tatu kwa kila shule ya sekondari umekamilika kwa kiwango
cha asilimia 95 mpaka sasa katika harmashauri ya wilaya ya Rungwe na shule
ambazo bado wapo katika hatua za mwisho za ujenzi wa maabara.
Na kuweka
azimo kwamba ifikapo tarehe ishirini na nane ya mwezi huu wanne shule zote za
halmashauri ya wilaya ya Rungwe ziwe zimekamilisha ujenzi huo kabla ya kufikia
agizo la Mhe. Rais la mwezi wa sita ili
kujipanga na ujenzi wa maktaba kwa kila shule.kwani serikali imetoa vitabu ishirini
na tano elfu vya sayansi katika shule za
Halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Akiongea na madiwani wa Halmashauri ya wilaya
ya Rungwe katika baaraza la madiwani mkuu wa wilaya Mhe.Chrispin Meela amesema
kuwa Ujenzi wa maktaba ni lazima ufanyike ili usaidie kuondokana na kutunza
vitabu kwenye ofisi ya mkuu wa shule kwani kunapelekea wanafunzi kutopenda
kusoma kama itakavokuwa vikiwekwa maktaba wanafunzi watakuwa huru kujisomea
muda wowote pamoja na siku za wikiendi.
Mhe.Meela
ameongeza kuwa matokeo ya darasa la nne kwa mtihani ulofanyika mwaka jana
Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imeshika nafasi ya kwanza katika Halmashauri
kumi na kwa darasa la saba Halmashauri imeshika nafasi ya pili kimkoa na
kiwango cha ufauru kimeongezeka na kufikia 51.2%.hivyo amewataka walimu wa
shule za msingi kuongeza juhudi katika ufundishaji ili kuongeza kiwango cha
ufauru na kufakia kiwango kama cha shule za sekondari zenye kiwango cha ufauru
wa 73%.
Mkuu wa
wilaya amewagiza madiwani na waratibu kata wa elimu kusimamia na kufuatilia ufundishaji
mashuleni kwa kutembelea shule na kukagua maandalio ya somo kwani walimu wengi
hufika mashuleni lakini hawafundishi na kukagua nidhumu za walimu hasa walimu
wapya, kwa walimu watakao kiuka wafikishwe kwa mgurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Rungwe na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
TUMAIN OBEL
KINGOTANZANIA
No comments:
Post a Comment