Staa wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Jide' na Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahaya Hussein.
Staa wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Jide'.
Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahaya Hussein.
Gladness Mallya na Gabriel Ng'osha
Habari njema! Kufuatia wimbi la baadhi ya mastaa kulia na tatizo la ugumba, mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahaya Hussein, amemtabiria mema staa wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Jide' kwamba endapo atatafuata tiba mbadala, atapata mtoto mwaka huu.
Akizungumza
na Ijumaa Wikienda, Maalim Hassan alisema kwamba, huu ni mwaka wa
mafanikio kwa Jide ambayo mwenyewe yatamshangaza likiwemo suala la mtoto
kama atachukua hatua ya kuwaona wataalam wa tatizo lake ambalo aliwahi
kulitoa kwenye kipindi chake cha Diary ya Lady Jaydee kupitia EATV la
jini mahaba.
Alieleza
kwamba jini mahaba huwa lina madhara makubwa kwa mwanamke na ndilo
linalowasumbua wengi kwani wanapima vipimo vyote hospitali na kuonekana
wana uwezo wa kuzaa lakini wanashindwa kutokana na tatizo hilo.
"Jide aje
kwangu nitamsaidia na ndani ya mwaka huu atapata mtoto maana nyota yake
inaonyesha mafanikio mengi au kama akishindwa kuja kwangu basi atafute
wataalam wa mambo ya majini, watamsaidia kwani hana tatizo la ugumba ila
kukosa kwake mtoto kunatokana na jini mahaba ambalo likimshika mwanamke
anajikuta akikosa mtoto," alisema Maalim Hassan.
Aliongeza
kwamba wasanii wengi wa kike wamekuwa wakilalamikia suala la kukosa
watoto japokuwa wengine wana tatizo hilo la jini mahaba huku wengine
wakitoa mimba na inapofika wakati wa kutaka watoto, wanakosa kwani mayai
yanakuwa yameisha.
CHANZO:GPL (Muro)
No comments:
Post a Comment