Mahmoud Ahmad Arusha
………………………………..
Imeelezwa kuwa elimu ya juu inaweza kuchangia watu wote
kupata elimu hapa nchini ikiwemo matumizi ya simu za mkononi na
utandawazi kama matumizi sahihi ya teknolojia na kuwafikia wananchi
wengi hata vijijini.
Kauli hiyo imetolewa na makamu mkuu wa Taasisi ya Nelson
Mandela Prof.Botrun Mwamila wakati wa hitimisho la mkutano uliondaliwa
na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na serikali ya Sweden na vyuo vikuu vya
nchi hiyo uliofanyika chuoni hapa kwa siku tatu kujadili teknolojia
inavyoweza kusaidia kuweza kupata elimu.
Prof.Mwamila alisema kuwa elimu ya vyuo vikuu kama
itatumiwa vizuri na wasomi wetu hapa nchini inaweza kuwasaidia wananchi
wengi wa madaraja yote kuweza kupata elimu kusudiwa na hivyo kuweza
kurahisisha maendeleo na ukuaji wa kiuchumi.
Alisema kuwa katika mkutano huo wamejadili mambo mbali
mbali yatakayosaidia kuweza kutoa elimu kwa urahisi kuwafikia wananchi
kwa kutumia teknolojia ya simu za mkanoni ambazo wananchi wengi wanazo
hata vijijini.
“Teknolojia na utandawazi ukitumiwa vizuri unaweza kusaidia
katika ukuaji na upatikana wa elimu hivyo kuondoa matatizo yatokanayo
na wananchi kutoweza kupata elimu na kushindwa kuchangia shemu ya
maendeleo”alisema Prof.Mwamila.
Aidha alisema kuwa maazimo yaliotokana na mkuatano huo
yatakuwa ni sehemu ya Agenda ya mkutano utakaofanyika nchini Korea
Kusini ambapo suala la elimu kwa wote bila ya kujali jinsia litapewa
kipaumbele katika majadiliano ya mkutano huo.
Akatanabaisha kuwa ukuaji wa elimu na matumizi ya
utandawazi ikiwemo simu za mkononi na matumizi ya mtandao wananchi
wakiacha kutumia kwa matumizi yasiofaa na wakageukia kutumia kwa
kujipatia elimu maendeleo ya haraka yatapatikana hapa nchini na hivyo
kila mwananchi kwa daraja lake atasogea kiufahamu.
No comments:
Post a Comment