Saturday, June 27, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE, MAKAMU WAKE DKT. BILAL WAWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA GEITA, VIWANJA VYA KARIMJEE, DAR SE SALAAM

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Picha zote na OMR
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete,  akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
3
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Juni 27, 2015 kwa ajili ya kushiriki shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max.
6
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Makamu wa Dkt. Bilal, wakati walipokuwa katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
7
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Bilal, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na baadhi ya Viongozi wakijumuika na waombolezaji katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
8
Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
9
Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
10
4
Post a Comment