Monday, June 22, 2015

TASAF WATOA MAFUNZO YA KUTEKELEZA MIRADI YA KUTOA AJIRA YA MUDA KWA JAMII YA KAYA MASKINI.


DAS WA WILAYA YA RUNGWE MOSSES MASHAKA AKIFUNGUA MAFUNZO YA KUNUSURU KAYA MASKINI WILAYANI RUNGWE TASAF AWAMU YA TATU

CHRISTOPH SANGA MKURUGENZI MKAGUZI WA NDANI WA TASAF MAKAO MAKUU AKITOA HOTUBA YA UFUNGUZI WA MAFUNZO KWA WATENDAJI NA WAKUU WA IDARA WA HALMASHAURI YA RUNGWE NA BUSOKELO KATIKA UKUMBI WA JOHN MWANKEJA TUKUYU MJINI






PICHA YA PAMOJA



Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) awamu ya tatu wameanza kutoa mafunzo kwa wataalam wa  idara wa wilaya ya Rungwe kuhusu  utaratibu wa kutekeleza miradi ya kutoa ajira ya muda iliyo chini ya mpango wa kunusuru kaya masikini kwa lengo la kujenga timu ya wataaramu ngazi ya eneo la utekelezaji kuhusu miradi ya kutoa ajira ya muda  ya mipango jumuishi inayolenga hifadhi ya udongo na maji .

Akitoa ufafanuzi huo Mkurugenzi mkaguzi wa ndani wa TASAF Bwana Christopha Sanga katika kufungua mafunzo hayo amesema kuwa mpango wa kunusuru  kaya masikini ambao unafanyika kwa kipindi cha miaka kumi ambao umegawanywa katika awam mbili za miaka mitano mpaka sasa mamlaka za 161 za Tanzania bara na Tanzania Zanzibar tayari zimefikiwa na walengwa zaidi ya milioni moja wametambuliwa.

Aidha jumla ya walengwa 58,202 walishiliki katika  miradi  ya kutoa ajira ya muda katika jaribio lililofanywa  katika mamlaka ya eneo la utekelezaji  manane ambayo ni Chamwino,Bagamoyo, kibaha,manispaa ya lindi,halmashauri ya wilaya ya lindi,manispaa ya Mtwara Mikindani,Unguja na pemba ambapo  jumla ya miradi 549 imetekelezwa na miradi hiyo imeanza kutoa huduma iliyokusudiwa na kufikia Mei 2015  jumla ya TZS 6.9 billion zimelipwa kama ujira.

 Akifungua mafunzo hayo  Katibu tawala wa Wilaya ya Rungwe Bwana Moses Mashaka amesema kuwa  ni jambo la kushukuru TASAF kwani mpango umeweza kufanya  malipo  kwa walengwa kwa wakati, hadi kufikia mwezi Mei 2015 TASAF imefanya  awam tisa za malipo, ambapo jumla ya shilingi bilioni 50.4 zilishalipwe zililipwa kwa kaya  za walengwa 259,715.Na utaratibu uta husisha jamii katika hatua zote za miradi kwa kufanya mipango jumuishi na kusema kuwa  lengo ni kuona kwamba angalau katika nchi hii wananchi  weny chini wawe na kipato chana kipatro cha kati.

 Kwa upande wake Mratibu  wa TASAF wilaya ya Rungwe Bi.Lidia amesema kuwa TASAF awamu ya tatu wameweza kufikia vijiji  miamoja ishirini na sita (126) kwa halmashauri zote mbili yaani busokelo na Halmashauri ya wilaya ya Rungwe  na hawana idadi kamili ya walengwa  kutokana na mchakato unaoendelea. 

Kwa mkoa wa Mbeya  Mratibu wa TASAF mkoa amesema kuwa mpango wa kunusuru kaya masikini sana umeshaanza kutekelezwa ambapo zoezi la utambuzi tayari limefanyika katika Halmashauri zote za mkoa wa Mbeya na zoezi la uandikishaji kwa kaya zilizo hakikiwa limefanyika kwa Halmashauri zote isipokuwa  halmashauri ya Busokelo na Halmashauri ya Rungwe  na kusema kuwa Tunategemea vipato vya kaya masikini  vitaongezeka pale watakapo anza kupewa ruzuku.
 KINGOTANZANIA

No comments: