Thursday, July 30, 2015

HOSEA CHEYO KUMRITHI KIBONA JIMBO LA ILEJE 2020


 Mbunge wa Ileje anayetetea nafasi yake, Aliko Kibona akizungumza na wananchi wa kata ya Luswisi hivi karibuni.

 Mtangazaji wa TBC Mbeya Hosea Cheyo akitoa msaada wa fedha taslim kwa kikundi cha ngoma za asili wilayani Ileje.

 
 Hosea Cheyo akiwa na mmoja wa wazee wa Kata ya Luswisi wilayani Ileje wakibadilishana mawazo.

 Hosea Cheyo akiwa na baadhi ya wananchi wa Ileje wakiangalia burudani ya ngoma za asili.


Hosea Cheyo akiwa na viongozi wa kampuni ya Simu ya TTCL walivyotembelea Kata ya Luswisi.
 
MBUNGE wa Jimbo la Ileje anayetetea nafasi yake, Aliko Kibona, amewataka wananchi wa jimbo hilo kumuongeza miaka  mingine mitano ili akamilishe miradi ya maendeleo aliyoianza.
 

Aliyabainisha hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na wapiga kura  kuhusu adhma yake  yakutetea nafasi ya ubunge.
 
Aidha Kibona amesema baada ya kumaliza miaka mitano atawaletea mtu ambaye yeye anamuona anamapenzi mazuri na wakazi wa Ileje na anauwezo wa kurithi viatu vyake endapo atashawishiwa kugombea kiti hicho mwaka 2010.
 
Aliko Kibona mbali na kuomba kuongezewa muda na kuaandalia mgombea wananchi wa Ileje amepata upinzani mkali kutoka kwa wagombea wengine ambao ni Godfrey Kasekenya,Janeth Mbene,Lyson Mnkondya,Willium Ndile na Marcelin Ndibwa.
 
Alisema  miradi ambayo ameianza nab ado kukamilika ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa nyumba za walimu ambazo amekuwa akitafuta  misaada kutoka kwa wadau wa ndani na nje ili kuhakikisha walimu wanaishi katika mazingira mazuri ili kuboresha sekta ya elimu.
 
Aliongeza kuwa mbali na sekta ya elimu pia suala la umeme vijijini lipo katika  hali nzuri huku ujenzi wa barabara ya Lami kutoka Mpemba hadi Isongole  ikitarajiwa kuanza muda wowote baada ya  Waziri wa Ujenzi Dk. John

Magufuli ambaye aliahidi kuijenga anakuwa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa
Tanzania hivyo akiingia Ikulu atakutana na ahadi hiyo.
 
Akizugumzia mtu anayedhani anaweza kumrithi ifikapo 2020,Kibona alimtaja Mtangazaji  na mwakilishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)Mkoa wa Mbeya, Hoseah Cheyo.
 
Alisema katika vijana anaowaona wenye uchungu na Ileje ni Cheyo hivyo atatumia muda mwingi kumshawishi na kuanza  kumuandaa katika chaguzi za ndani za chama kuanzia mwaka 2017.
 
Alisema Cheyo ni mchapa kazi kwani utendaji wake na jinsi anavyoripoti habari

za Ileje zinaonesha kuwa na kiu yakuona watu wa Ileje wakipata maendeleo
ya haraka na kuwa Wilaya yenye mafanikio makubwa katika kipindi kifupi.
  
“Niseme kutoka ndani ya mtima wa moyo wangu mtu pekee ninae muona anaweza

kunirithi ni Osea Cheyo, niko tayari kumshawishi na kuanza kumuandaa
kuwa Mbunge kwenye uchaguzi wa ndani ya Chama 2017”alisema Kibona.
  
Kwaupande wake Cheyo alipoulizwa utayari wake wa kushikaUbunge wa Ileje

alisema anashauku kubwa ya kuwaletea maendeleo watu wa Ileje hivyo
wakati ukifika atakuwa tayari kama itampendezaMungu.
 
Aliongeza kuwa anatamani Wilaya ya Ileje ikiwa ni kitovu cha kilimo cha Kahawa isiyotumia madawa na mbolea za madukani hapa nchini na kuwa na wanunuzi kutoka pande zote za dunia jambo litakalochangia kupatikana kwa

maendeleo haraka ikiwemo miundombinu.
 

No comments: