Monday, August 24, 2015

MAGUFULI PELEKA SUNAMI KATAVI, MIKUTANO YAKE WE ACHA TU

1
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni wa Chama hicho uliofanyika kwenye uwanja wa Azimio mjini Mpanda mkoani Katavi  leo ambapo amehutubia mikutano ya hadhara mitatu katika mkoa huo  katika maeneo ya Mishamo, Katumba na Mpanda mjini.
Dr. Magufuli amewaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ili ashinde na  shughulika na matatizo ya wananchi  kwakuwa  anayaelewa matatizo na shida nyingi za watanzania, Dr. Magufuli ameahidi kukamilisha ujenzi wa barabara za Kasulu -Mpanda,  Sumbawanga – Mpanda , Mpanda -Tabora ili zikamilike kwa kiwango cha lami na kuwarahisishia wananchi katika shughuli mbalimbali za kiuchumi mkoani humo PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-KATAVI
2
Umati wa wananchi ukimsikiliza Dr. John Pombe Magufuli  hayupo pichani wakati alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni mjini Mpanda leo.
3
Dr. John  Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia wananchi katikia mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Azimio mjini Mpanda.
4
huu ndiyo umati ambao umehudhuria katika mikutano   mbalimbali yake ya Kampeni mkoani Katavi leo.
5 6 8 9
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimnadi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mpanda kwenye uwanja wa Azimio.
10
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye kata ya Katumba mkoani Katavi leo.
11
Baadhi ya wana CCM wakiwa wameshikilia mabango yenye picha ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la  Mishamo leo mkoni Katavi 
12
Wananchi wakimfurahia Dr John Pombe Magufuli wakati alipowasili katika eneo la mkutano wa Kampeni la Mishamo kata ya Ifumbula.
13
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akijadiliana jambo na mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli kabla ya kuhutubia kwenye mkutano wa kampeni mjini Mpanda.
15
Dr, John  Pombe Magufuli aki na msafara wake akiwasili katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Azimiao mjini Mpanda leo.
17
Dr, John  Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Katumba wilayani Mpanda mkoani Katavi.
19
Wananchi wakinyanyua mikoni yao juu juu kuonyesha kumkubali Dr. John Pombe Magufuli mgombea urais kupitia CCM wakati alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara eneo la Katumba.
20
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wananchi na kumuombea kura za ndiyo mgombea wa urais kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli hayupo pichani wakati akiwahutubia wananchi wa eneo la Katumba mkoani Katavi.
21
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kulia akiwa ameketi meza kuu pamoja na Mgombea urais kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni eneo la Katumba mkoani Katavi kushoto ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Ndugu William Likuvi.
22
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kulia akiwa  meza kuu pamoja na Mgombea urais kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli  wakiimba wimbo kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni eneo la Katumba mkoani Katavi wa tatu kutoka kushoto ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Ndugu William Likuvi
23
Umati wa wananchi ukiwa umejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la Mishamo Mchana wa leo mkoani Katavi.
24 25
29
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimnadi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni wa Chama hicho uliofanyika eneo la Mishamo kata ya  
30
Wananchi wakiwa wameshikilia mabango yenye picha za mgombea urais kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli huku wakipunga mikono yao juu katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mishamo Mkoani Katavi
31 32
Vaadhi ya wananchi mbalimbali wakifuatilia hotuba za mgombea urais kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwasalimia maeneo mbalimbali aliyopita.
33
Wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba za Dr. John Pombe Magufuli wakati akiwaomba kura katika moja ya mikutano yake ya kampeni mkoani Katavi leo.
34
Dr. John Pombe Magufuli wakati akiwaomba kura wananchi katika moja ya maeneo mbalimbali aliyopita na kuzungumza na wananchi akiwa kampeni zake za kuingia ikulu mkoani Katavi leo. 
35
Wananchi mbalimbali wakimshangilia Dr. John Pombe Magufuli .
37
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimsalimia mtoto Ruby aliyekuja na Mama yake kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kwa ajili ya kumpokea mgombea huyo wakati alipowasili mkoani humo kwa ajili ya kampeni.
Post a Comment