Wednesday, August 19, 2015

Mgombea Urais wa Chadema, EDWARD LOWASSA na Mwenza wake DUNI HAJI, wasaini Hati ya Kiapo

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisaini fomu za
hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania,
Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Hati ambayo kila mgombea wa
nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es
Salaam ili kuthibitisha usahihi wa fomu hizo kabla ya mkuzirejesha Tume
ya Taifa ya Uchaguzi, kwa uteuzi. Kushoto ni Mgombea Mwenza, Juma Haji
Duni, maarufu kama “Babu Duni”
 
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni
akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya
Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Kushoto kwake ni
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama
hicho, Mh. Edward Lowassa.
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza
wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwa kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya
Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu (mbele) wakati wa kusaini fomu za hati
ya Kiapo, leo Agosti 19, 2015. Kulia ni Mwanasheria wa CHADEMA, Mh.
Mabele Marando.
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za
hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman
Said Komu.
 
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni
akipokea fomu za hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania,
Jaji Suleiman Said Komu. Kulia ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa.
 

No comments: