Saturday, October 24, 2015

Tanzania (Bloggers) tumejadiliana na kukubaliana kwa pamoja kuhusu hatma na mustakabali wa taifa letu kuhakikisha amani na utulivu vinadumishwa wakati na baada ya uchaguzi huu wa kidemokrasia na kwa kauli moja tumetoa msimamo wetu kuhusu amani ya nchi hii.  Kwa ujumla, hakuna anayeweza kujisifu kuwa ana uhalali zaidi wa taifa hili kuliko mwingine, taifa hili ni letu sote, hivyo wajibu wa kulinda na kudumisha amani na usalama wa nchi ni wa kila mmoja.  Tunaomba Watanzania wote wenye sifa wajitokeze kupiga kura kwa amani na utulivu, wasubiri matokeo kwa amani na utulivu, wapokee matokeo kwa amani na utulivu, maisha yaendelee kwa amani na utulivu, tusonge mbele kwa amani na utulivu huku tukijua kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi, na hilo ndilo muhimu zaidi.  MUNGU IBARIKI TANZANIA! 

Post a Comment