Monday, December 7, 2015

TAARIFA YA WAZIRI MKUU KWA WATANZANIA ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE

1 
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa  akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo wakati alipotoa taarifa ya serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi wa TPA, TRA, Wizara ya Uchukuzi na TRL. kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni Sefue.
3 
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wa kwa utulivua wakati akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari , Kalia ni Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue.
4 
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa akiingia kwenye ukumbi wa mikutano tayari kwa kuzungumza na  waandishi wa habari.
…………………………………………………………………………………………………………….
Mnamo tarehe 27 Novemba, 2015 nilifanya ziara ya kushitukiza Bandari ya Dar es Salaam ambapo nilifichua mwanya wa ukwepaji kodi kwa makontena 329 yaliyopitishwa bandarini kinyume cha utaratibu.
Mtakumbuka pia tarehe 4 Desemba, 2015 nilirudi tena kufanya ufuatiliaji wa hatua ya udhibiti wa upitishaji wa bidhaa mbalimbali kinyume cha utaratibu.
Ziara yangu ilinipitisha hatua zote za upitishaji mizigo ambazo pia kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi wa Ndani wa tarehe 30 Julai 2015 Mamlaka ya Bandari uligundua kuwepo kwa mianya mingi ya ukwepaji kodi ikiwemo na makotena 2387 yaliyopitiahwa kati ya Machi – Septemba 2014 kinyume cha utaratibu, vitendo hivi vinaonyesha kuwa bandari yetu hupitisha makontena mengi bila ya kulipiwa kodi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.
Upotevu huo unaenda sambamba na mfumo usiokidhi wa kupokelea malipo (BILLING SYSTEM) ambao unatoa mwanya mkubwa wa kupoteza mapato ya Serikali. Bandari ni eneo muhimu ambako kama panasimamiwa vizuri panaweza kukusanya fedha nyingi na kuchangia Pato la Taifa.
Serikali haitavumilia kuona watu wachache au kikundi chochote kilichojipanga kuhujumu mifumo au kuiibia Serikali kwa namna yoyote ile kwa manufaa ya wachache.
Matokeo ya ziara hizo ni haya yafuatavyo:-
1. Nimeagiza mfumo wa kupokelea malipo ubadilishwe kutoka Billing System na uwekwe mfumo wa e-payment ambao tayari ulianza kuwekwa na uwe umekamilika kufikia tarehe 11 Disemba 2015.
2. Kwa kuwa ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji makontena hayo na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, kuanzia muda huu nawasimamisha kazi wale wote waliohusika kupitisha makontena kinyume na utaratibu.
1. Wasimamizi wa Bandari Kavu (ICD)
(i) Happygod Naftari
(ii) Juma Zaar
(iii) Steven Naftari Mtui
(iv) Titi Ligalwike
(v) Lydia Prosper Kimaro
(vi) Mkango Alli
(vii) John Elisante
(viii) James Kimwomwa – ambaye amehamishiwa Mwanza.
2. Wafuatao ni Viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya Bandari ambao hawamo kwenye ripoti ila ni wahusika wakuu.
1. Shaban Mngazija – Aliyekuwa Meneja Mapato ambaye kwa sassa amehamishiwa Makao Makuu kitengo cha Fedha.
2. Rajab Mdoe – Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu (ICD) – ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi Co-operate Services.
3. Ibin Masoud – Kaimu Mkurugenzi wa Fedha.
4. Apolonia Mosha – Meneja Bandari Msaidizi – Fedha.
5. James Kimwomwa.
Kutokana na utendaji mbovu wa Mamlaka ya Bandari kwa muda mrefu na kwa kitendo cha kutochukua hatua kwenye vyanzo.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amevunja Bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa wafuatao:-
1. Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari – Prof. Joseph Msambichaka.
2. Mkurugenzi Mkuu wa Bandari – Bw. Awadhi Massawe.
Ndugu Waandishi wa Habari mtakumbuka pia nilifanya ziara pia TRL ambako kwa awali nimegundua matumizi mabaya ya fedha Shilingi Bilioni 13 nje ya utaratibu ambako uchunguzi unakamilishwa.
Mheshimiwa Rais, pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia tarehe ya leo na atapangiwa kazi nyingine.
Post a Comment