Monday, February 1, 2016

GHALA LATEKETEA KWA MOTO NA MALI ZILIZOKUWEMO.


 
Geti la kuingilia kwenye ghala lililoteketea kwa moto


Gari la polisi maarufu kwa washa washa likisaidia kuzima moto tofauti na ilivyozoeleka kuwa linatumika katika kuondoa vurugu

Vikosi vya uokoaji vikiendelea na zoezi la kuzima moto

Baadhi ya bidhaa zikiwa zimesambaa chini katika ajali ya moto


GHALA la kuhifadhia bidhaa mbali mbali za vyakula ukiwemo unga na mafuta ya kupikia limeteketea kwa moto eneo la Forest jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema moto huo ulianza kuwaka majira ya asubuhi leo na kuteketeza baadhi ya vitu kabla ya Jeshi la zimamoto na uokoaji hawafika.

Mashuhuda hao ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema ghala hilo ambalo getini kumeandikwa jina la Azania haijafahamika chanzo cha moto huo na kuongeza kuwa waliona moshi mkubwa ukitoka katika eneo hilo.

Walisema taarifa za awali zinadai kuwa mmiliki wa ghala hilo ndiyo yule Yule aliyewahi kuunguliwa na ghala lingine kipindi cha nyuma karibu na uwanja wa ndege wa zamani(Airport).

Hadi tunaingia mtamboni hakuna taarifa iliyotolewa juu ya hasara iliyopatikana katika ajali hiyo hata majeruhi.
Post a Comment