Monday, May 8, 2017

AFYA YAKO. Jinsi Ya Kugundua Na Kuthibiti Vidonda Vya Tumbo( Peptic Ulcer)


Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwishoni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni'Gastric Ulcer'vikiwa katikati ya sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo ni 'Duodenal Ulcer' na vikiwa katika koromeo tunaita 'Esophageal Ulcer'.

NINI HUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO:
Kisababishi kikuu ni bacteria aina H.Pylori Helicobacter Pylori ambaye hupatikiana kupitia vyakula na maji,pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo haswa kwa wenza wanaonyonyana ndimi. Bacteria hawa huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimen'genya viitwayo. Urease inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo,utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo, idadi kubwa ya watu wenye vidonda pia wana ndugu wenye vidonda vya tumbo,uvutaji sigara na tumbaku pamoja na unywaji pombe pia husababisha vidonda na msongo wa mawazo pia.

DALILI:
Ni nadra sana kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo kutoonyesha dalili kama maumivu makali ya tumbo aidha usiku.ukiwa na mawazo,ukiwa na njaa au ukishiba sana(maumivu haya huanzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua),kushindwa kumeza chakula au kukwama kama kinataka kurudi,kujisikia vibaya baada ya kula,kupungua uzito,kukosa hamu ya kula,kutapika damu,kupata choo cheusi chenye damu,kuhisi kutapika.

JINSI YA KUGUNDUA NA KUDHIBITI VIDONDA VYA TUMBO
Maelezo ya mgonjwa kuhusu dalili humwezesha daktari kuhisi kinachomsumbua mgonjwa kuwa ni aina gani ya vidonda vya tumbo aidha peptic ulcers,gastric ulcer,duodenal ulcer au esophageal ulcer.
Ili kuthibitisha aina ya vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika

  • Kupima damu kuangalia bacteria aina ya h.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibiotic au dawa za vidonda'proton pump inhibitors-PPIs mfano. Omeprazole'vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi.
  • Kupima pumzi:mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjia,hii hufanya bacteria ya H.pylori kuvunjika na baada ya saa moja mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa na endapo mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.
  • Kupima antigeni kwenye kinyesi,kuangalia kama kuna bacteria h.pylori kwenye kinyesi
  • Kufanya x-ray ya sehemu ya juu ya tumbo'upper gastrointestinal x-ray'picha huonyesha esophagus,mfuko wa tumbo'stomach'na duodenum


JINSI YA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO
 Baada ya kufahamu kwa kina vyanzo vya vidonda vya tumbo,aina ya vidonda vya tumbo,dalili ya vidonda vya tumbo,uchunguzi/vipimo ni vyema tufahamu mambo yatakayotusaidia kuishi vizuri tukiwa na vidonda vya tumbo.

  • Awali ni vyema mhanga aache kabisa kutumia kahawa na chai kwani huongeza kiwango cha asidi kinachotenezwa na tumbo lako(unaweza kutumia mchaichai kama mbadala).
  • Jitahidi kupunguza uzito hasa ikiwa uzito umezidi na hauendani na kimo chako.
  • Kula angalau kidogo mara kwa mara,hii itasaidia kupunguza athari za asidi inayotengenezwa na tumbo.
  • Epuka kunywa pombe na vileo kwani hutonesha kwenye vidonda vinavyotaka kupona.
  • Epuka matumizi ya viungo vya vyakula kwani yana gesi/asidi nyingi,Acha kabisa kuvuta sigara kwani hukuweka kwenye hatari zaidi ya vidonda kuanza upya au kuzuia vidonda.

Mpenzi msomaji wa makala hii yawezekana wewe ama ndugu ama rafiki yako ni mgonjwa na anasumbuliwa na tatizo hili, na ametumia madawa mengi bila kupona. Basi napenda kukupa habari njema kuwa tumefanikiwa kutengeneza vidonge kwa kutumia mimea ambayo inatibu na kuondoa tatizo hili.
.

No comments: