Sunday, May 14, 2017

Mtu wa 30 auawa kwa Risasi Kibiti Mkoani Pwani

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bungu wilayani Kibiti, Alife Mtulia ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha.

Kamanda Lyanga amesema mauaji hayo yamefanyika usiku wa kuamkia leo (Jumapili) katika Kijiji cha Nyambunda. Amesema Mtulia aliuawa na watu hao alipokuwa anakwenda kuoga.

Kamanda amesema mwili wa marehemu umepelekwa kituo cha afya cha Kibiti kwa uchunguzi.
Mauaji ya askari Polisi, viongozi wa Serikali za Mitaa na raia yamekuwa yakifanyika mara kwa mara katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.

Jumanne wiki hii akiwasilisha bungeni bajeti ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba aliliambia Bunge kuwa Serikali itaanzisha mkoa mpya wa kipolisi katika wilaya za Kibiti, Rufiji, Mkuranga na Mafia ili kuimarisha ulinzi.

Kwamujibu wa rekodi za matukio ya mauji katika mkoa huo mpakaka sasa wanafikia watu 30 waliokwisha uawa

No comments: