Saturday, May 13, 2017

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini yaharibu mawasiliano kati ya Bukoba na Mwanza

 Mvua imesababisha barabara kuu ya Mwanza -Bukoba kukatika eneo la Kemondo, hivyo magari ya abiria na mizigo kuzunguka Kyetema kupitia Katerero kutokea Muleba.

Barabara hiyo ilikatika jana  (Ijumaa) saa 11:00 alfajiri kutokana na mvua iliyonyesha usiku kucha na kusababisha maji kujaa kwenye karavati.

Kutokana na hali hiyo wananchi na hasa wafanyabiashara wa eneo la Kemondo wameshindwa kuendelea na shughuli zao kwa kukosa mawasiliano.

Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Kagera, Andrew Kasamwa amesema watumiaji wa barabara hiyo wanatumia njia mbadala kwa kupita Katerero mzunguko wa umbali wa takriban kilomita 10.
Amesema jitihada zinafanywa kukarabati eneo hilo ili kurejesha mawasiliano.

Post a Comment