Wednesday, May 10, 2017

Trump amfuta kazi mkurugenzi wa FBI James Comey

Rais Trump na james Comey wa shirika la FBI wakisalimiana katika mkutano wa awali

Lakini wanachama wa Democrats wamesema kuwa alifutwa kazi kwa sababu FBI ilikuwa ikuchunguza madai ya uhusiano kati ya Trump na Urusi.
Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba bwana Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la Congress wiki iliopita.
Rais Trump aliandika barua kwa bwana Comey kwamba alikubaliana na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba ameshindwa kuliongoza vizuri shirika hilo.
Bwana Sessions alisema kuwa idara ya haki ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu na sheria na mwanzo mpya unahitajika.
Naye kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, Bwana Chuck Schumer, amesema kuwa ni wakati mwafaka sasa kumteua kiongozi maalumu wa mashtaka kusimamia uchunguzi huo juu ya uhusiano na Urusi.
Alisema kuwa hatua hiyo isipochukuliwa raia wa Marekani wana haki ya kuwaza kuwa Bwana Comey amefutwa ili kupunja juhudi za kukamilisha uchunguzi huo.
Ikulu ya White House imekanusha kuwa kutimuliwa kazini kwa Bwana Comey kuna uhusiano wowote na maswala ya kisiasa.Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa utafutaji wa mrithi wake unaanza mara moja.

KINGOTANZANIA

No comments: