Tuesday, May 23, 2017

Uingereza yaimarisha ulinzi baada ya watu 22 kufariki DUNIA


Haki miliki ya picha
Uingereza itasambaza wanajeshi kwa ajili ya kulinda maeneo muhimu na kwenye matukio mbalimbali, kufuatia shambulio la kigaidi lililotokea katika mji wa Manchester na kusababisha vifo vya watu 22.
Hatua hiyo isiyo ya kawaida imetangazwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo Theresa May, ambaye amesema ukadiriaji unaofanywa juu ya kitisho cha ugaidi kinachoikabili nchi hiyo, umeongezwa kwa kiwango kikubwa.
Ikiwa na maana kwamba mashambulio ya kigaidi yanaweza kutokea tena.
Waziri mkuu wa Uingereza amesisitiza kuwa kuna uwezekano wa kundi la watu lina weza kuwa na uhusiano na shambulio la Jumatatu usiku la Manchester.
Post a Comment