Thursday, June 1, 2017

Waziri Mkuu Mjaliwa: Uchunguzi makinikia haujakamilika

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji nchini kuondoa hofu kwani kamati ya pili iliyoundwa kufanya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini (makinikia) bado haijakamilisha kazi yake.

Majaliwa amebainisha hayo leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka aliyetaka kujua hatma ya zuio la usafirishaji wa makinikia hayo.

"Mpaka sasa tumepokea taarifa moja na bado tunasubiri taarifa ya pili katika hili nataka niwasii wawekezaji wote kwanza wasiwe na mashaka kwa sababu lengo la serikali ni kujiridhisha tu kwamba je mchanga huu unaosafirishwa kwenda nje una nini na hatu bugudhi uzalishaji wao. Baada ya kuwa tumepata ile taarifa ya kwanza bado hatua kamili hazijachukuliwa tunasubiri taarifa ya kamati ya pili baada ya hapo sasa serikali itaka chini na kutafakali kwa kupata ushauri kutoka sekta mbalimbali za kisheria, kiuchumi na maeneo mengine hatua gani tuchukue kwa hiyo nitoe rai hata kwa watanzania wawe watulivu wasuburi majibu ya serikali ambayo yatalinda haki ya kila muwekezaji" alisema Majaliwa.

Pamoja na hayo, Mhe. Majaliwa amesema endapo serikali itashindwa kujenga mitambo ya kuchenjua makinika itakaribisha wawekazaji ili waweze kufanikisha ujenzi huo.
Post a Comment