Monday, July 3, 2017

FAO: Idadi ya watu wenye njaa duniani yaongezeka

Idadi ya watu wenye njaa duniani imeongezeka tangu mwaka 2015 na hivyo kurejesha nyuma mafanikio yaliyopatikana katika kuondokana na tatizo hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva amesema hayo huko Roma, Italia wakati akifungua mkutano mkuu wa wa siku sita wa shirika hilo unaofanyika kila baada ya miaka miwili.

Amesema takribani asilimia 60 ya wakazi wenye njaa duniani wanaishi kwenye nchi zinazokumbwa na mizozo na mabadiliko ya tabianchi, akitaja nchi 19 zilizo na mizozo isiyoisha.

Miongoni mwao ni Somalia, Nigeria na Sudan Kusini akisema awatu milioni 20 kwenye nchi hizo zaidi ya kukabiliwa na njaa, wamesalia hohehahe kwa kuwa hawawezi kujihusisha na shughuli za kujipatia kipato.

"Njaa itatokomezwa iwapo tu nchi zitabadili ahadi zao kuwa vitendo hasa katika ngazi ya kitaifa na kimitaa. Huko ndiko watu wanahitaji.Leo hii mizozo na athari za mabadiliko ya tabianchi vinaendelea kuongeza changamoto za juhudi za kimataifa kutokomeza njaa na ufukara"
Post a Comment