Tuesday, November 21, 2017

Rais Robert Mugabe hatimaye amejiuzulu

Rais Robert Mugabe amejiuzulu

Image captionRais Robert Mugabe amejiuzulu
Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .
Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.
Nukuu ya rais Mugabe alipokuwa akijiuzuluHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionNukuu ya rais Mugabe alipokuwa akijiuzulu
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano.
Raia wa Zimbabwe wafurahia kujiuzulu kwa MugabeHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRaia wa Zimbabwe wafurahia kujiuzulu kwa Mugabe
Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.

No comments: