Wednesday, July 18, 2018

Serikali yatumia Sh Bilioni 150 kulipa wastaafu


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Ajira Vijana na watu wenye ulemavu, Jenister Mhagama amesema serikali inaendelea kufanya uchambuzi wa kubaini watumishi wote waliostaafu kabla ya 1999 ambao walikuwa wakichangia katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili waweze kulipwa madai yao ambapo mpaka sasa shilingi Bilioni 150 zimeshalipwa.

Akizungumza na watumishi wa Chama cha Walimu Tanzania CWT kwa niaba ya Waziri Mhagama,Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi ajira na vijana Mhe Antony Mavunde amesema ni dhamira ya serikali kuhakikisha wastaafu wote wakiwemo walimu wanalipwa madai yao.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Walimu Tanzania CWT Mwalimu Leah Ulaya amesema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya baadhi ya vyama vinavyopingana na CWT hivyo kuleta migogoro ndani ya chama hali inayowafanya wananchama kushindwa kupata haki zao za msingi.

Naye Katibu Mkuu wa CWT Taifa Mwalimu Deus Seif amesema kuwa walimu wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinapelekea baadhi ya walimu kutekeleza vyema majukumu yao huku wakiomba serikali kuipa kipaumbele kada hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

No comments: