Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba hii leo amehitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Singida na kuwasili katika Mkoa wa Tabora, ikiwa ni mwendelezo wa kukagua, kutathmini, kuzungumza na viongozi, na wananchi kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, sambamba na uanzishwaji na ufuatiliaji utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi Mazingira ya mwaka 2004 katika ngazi za Serikali za Mitaa.
Katika siku ya tatu ya ziara yake Makamba ametembelea vichaka vya Itigi ‘Itigi thicket” na kupata fursa ya kuzungumza na viongozi wa wilaya ya Manyoni juu ya namna bora ya kuhifadhi eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 410,000 na kuahidi kutuma wataalamu kuandaa andiko la Mradi utakaonufaisha wakazi wa eneo hilo katika sekta uvunaji wa asali kwa njia ya kisasa zaidi.
“Ndani ya muda mfupi nitatuma wataalamu wangu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, waje wakae na wataalamu wenu na kuandaa Mradi utaonufaisha wakazi wa wanaozunguka eneo lote la msitu ili kutunza na kuhifadhi rasilimali za asili zilizopo katika eneo hili” Makamba alisisitiza.
Katika hatua nyingine Waziri Makamba amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bi. Rahabu Jackson kuwasilisha kwake majina wa watalaamu wa Mazingira ambao wana sifa za kuwa Wakaguzi wa Mazingira ili waweze kuteuliwa kwa mujibu wa Sheria.
No comments:
Post a Comment